Mshindi ashindani, Anafanyaje?

Eugen TZA

Member
Aug 7, 2023
61
98
Mshindi ashindani kwa kuwa ameshinda kabla ya kushindana, aliyeshindwa anashindana kwa kuwa ameshindwa kabla ya kushindana, Ushindi sio mchezo ni kilichopo nyuma ya mchezo, mbinu, maarifa, utashi na uelewa wa kanuni zilizo nyuma ya michezo.

Ukiuelewa mchezo hauna tena maana kwa kuwa umeshinda mbele za washindani wako, Washindi hawashindani wanajifunza kushinda kabla ya mashindano, Mashujaa sio walioshinda vitani bali wenye uwezo wa kuviepuka vita kwa kuwa havina budi kuwapo.

Mshindi ashindani na walioshindwa bali walioshinda ili apate kushinda nakwambia Mshindi ashindani na walioshinda bali wenye kushinda wakishinda kwa kuwa ushindi ni ule usio na fainali, Hakuna ligi nakwambia katika ulimwengu wa washindi bali walioshindwa.

Ni malipo gani yafaa katika ukamilifu, Hakuna kikombe wala taji kwa Mshindi bali walioshindwa, Hakuna faraja kwa wavumilivu bali upendo, Hakuna tamaa kwa aliye na vyote bali utukufu, Hakuna hamasa kwa walio hai bali waliokufa, Anayejua anachokitaka amekipata.

Mshindi ashindani kwa ajili ya vikombe wala mataji, Mshindi anashinda kwa kuwa amezaliwa mshindi juu ya mashindano, Mshindi ni bingwa katika ubingwa wa mabingwa, Mshindi ni mchezo unaowachezesha walioshindwa, Mshindi ni kanuni, muamuzi na uwanja.

Mshindwa anashindana kwa ajili ya vikombe na mataji, Mshindwa ameshindwa kwa kuwa ajazaliwa mshindi juu ya mashindano, Mshindwa ni bingwa bila ubingwa wa mabingwa, Mshindwa sio mchezo bali mchezaji wa walioshinda, Mshindwa ni tamaa, shabiki na hadhira.

Ushindani ni ushetani bila maarifa, Maarifa ni ushindi bila ushindani, Ushetani ni ushindani bila maarifa, Ushindani ni machafuko bila ushindi, Ushindi sio ushindani bali ukamilifu, Aliyeshinda ashindani na walioshindwa, Walioshindwa wanashindana na aliyeshinda.

Wasioshinda wanaimani watamshinda aliyeshinda, Mwenye imani ashindani na walioshindwa, Aliyeshinda anaimani ameshashinda, Aliyeshinda ni mwenye kushinda bila kushindwa, Aliyeshindwa ni mwenye kushindwa bila kushinda, Aliyeshinda ni aliyeshindwa kushindwa.

Mshindi ashindani bali walioshindwa, Mshindi ashindani anafanyaje???

Mshindi ashindani anashinda, Mshindi apigani anapiga, Mshindi agongani anagonga, Mshindi hawazi anawazwa, Mshindi ashikani anashika, Mshindi aungani anaunga, Mshindi akulani anakula, Mshindi abishani anabisha, Mshindi achezei anacheza, Mshindi achagui anajua.

Mshindwa anashindana hashindi, Mshindwa anapigana hapigi, Mshindwa anagongana hagongi, Mshindwa anawaza hawazwi, Mshindwa anashikana hashiki, Mshindwa anaungana haungwi, Mshindwa anakulana akuli, Mshindwa anabishana abishi, Mshindwa anachezea achezi, Mshindwa anachagua hajui.

Mshindi ashindani bali walioshindwa, Mshindi ashindani anafanyaje???

#PeaceOverInterest
 
Back
Top Bottom