Mshamu njoo CHADEMA ugombe ubunge Selina kombani hatufai

kijenge

Senior Member
Mar 9, 2012
179
164
Mshamu aliyekuwa mgombea udiwani kwa tiketi ya cuf ni mtu mahiri mchapakazi mtetezi wa wanyonge hapa ulanga.kwa kuwa cuf imekufa njoo cdm kwanza hustaili kugombea udiwani gombea ubunge mama selina kombani hana ubavu wa kupambana nawe2.tuna kero kibao amefumbia macho mahenge maji yanatiririka milimani lakini majumbani maji hakuna mahenge haijawahi kukosa mvua lakini ni moja ya wilaya zenye njaa tanzania.mlo wa mwanchi wa mahenge ni mlo mmoja kwa cku utazani hakuna mbunge.
 
Huyo Mshamu yuko humu?? Maana ninavyojua watu wengi hawapendi kuwa katika mitandao ya kijamii kama hii! Kama yupo tungependa kusikia anasemaje juu ya ombi hilo.
 
Huyo Mshamu yuko humu?? Maana ninavyojua watu wengi hawapendi kuwa katika mitandao ya kijamii kama hii! Kama yupo tungependa kusikia anasemaje juu ya ombi hilo.

Na hata kama yuko humu inawezekana hapendi ubunge yeye anapenda udiwani zaidi....
 
Jitokezeni wengi wananchi wataamua,wapo wengi ndani ya CDM hapo Ulanga wnye uwezo kuliko huyo Bwana!
 
Hivi huyu Celine Kombani si ndiye aliyemkondishia majambazi mgombea wa CDM yakamunyang'anya fomu zake za kugombea ubunge siku ya mwisho wakati akizipeleka kwa msimamizi wa uchaguzi. Matokeo yake Celine Kombani akapita bila kupingwa.

Naomba mnisahihishe kama nimekosea?!
 
ndiyo huyo pia alimuekea mgombea mwenzie wa magamba meno ya kiboko anaitwa azizi mpaka leo anakesi hapo ulanga na selina amedai mpka amfunge ili iwe fundisho kwa atakae mpinga hapo ulanga.na anaweza kwa kuwa yeye ni boss wa mahakama.na anayeza kuvuka mbinu hizo chafu za mama ni mshamu.
 
Jamani huyu Mshamu ndo yule nilisoma naye au???

inawezakana kama ulisoma na mtu anayeitwa mshamu shabani mbunda anaishi mahenge mjini kwa sasa ni mjasiriamali maarufu hapo mahenge.
 
Ishu ya udiwani alipata kura ngapi? maana inaonyesha kura za udiwani hazikutosha au aje abebwe na jina la CDM??????
 
Ishu ya udiwani alipata kura ngapi? maana inaonyesha kura za udiwani hazikutosha au aje abebwe na jina la CDM??????
Nadhani huko Mahenge kuna wana CDM ambao wanaweza kupeperusha vema bendera ya CDM kuliko huyo Mshamu. Hawa watu wanaojiunga ktk vyama ili wapate vyeo na madaraka ni hatari sana!
 
kama watu wa ulanga wamemwona anawafaa na cdm wanaona anafaa kusimamia sera za chama apokelewe na kuandaliwa mapema kiakili na kisera, makamanda lazima wawe tayari kwa vita muda wote, tusipuuze maoni ya watu kama magamba cdm kila taarifa, ombi, wazo, maoni, challenge(kupinga jambo) ni muhimu naomba viongozi wa wilaya mkoa taifa wafanyie kazi taarifa hii.
Ilimradi Mshamu nae awe tayari kwa mabadiliko kupitia peoples poooower...
 
Hakuna muda wa kubembelezana, Andaeni maandamano mpaka nyumbani kwake mkamueleze ni nini mnachokitaka, nendeni na waraka wa maandishi kabisa kabisa.

kama mkienda asubuhi mkakuta kaisha ondoka kwenda kwenye utafutaji wekeni kambi mpaka arudi akichelewa sana acheni waraka huyo nyumbani kwake kisha siku inatofuatia asubuhi mnaamkia kwake mpaka kieleweke.

Muelezeni ukweli kwamba yeye kama mwana ulanga anawajibika kuitumikia Jamii hiyo kwa ufanisi dhaidi na mmeonelea kwamba atawafaa kuwa mbunge wenu, na mumueleze wazi kwamba hamna Imani na CCM wala CUF sababu mambo yanayofanyika kwenye ngazi za kitaifa za vyama hivyo viwili hayajajielekeza katika kutatua kero za wananchi.

Asipowaelewa naweni mikono yenu hapo hapo nyumbani kwake muondoke lakini mumueleze kwamba mnachukulia kama kikwazo cha maendeleo yenu.
 
Mshamu aliyekuwa mgombea udiwani kwa tiketi ya cuf ni mtu mahiri mchapakazi mtetezi wa wanyonge hapa ulanga.kwa kuwa cuf imekufa njoo cdm kwanza hustaili kugombea udiwani gombea ubunge mama selina kombani hana ubavu wa kupambana nawe2.tuna kero kibao amefumbia macho mahenge maji yanatiririka milimani lakini majumbani maji hakuna mahenge haijawahi kukosa mvua lakini ni moja ya wilaya zenye njaa tanzania.mlo wa mwanchi wa mahenge ni mlo mmoja kwa cku utazani hakuna mbunge.

Mambo ya ajabu hayo, kwani huyu Mshamu ndo atawalimia mashamba yao? kama kuna njaa kwa uvivu wa watu kulima hata aje huyo Mshamu ni kazi bure... labda kama ndo kudanganyana atawalimia.....na kama yeye ni kiongozi mzuri basi hata akiwa hapo cuf mchagueni usilete kampeni za uongo ujanja
 
Back
Top Bottom