Mshambuliaji Thomas Ulimwengu kufanya Majaribio AS Monaco

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733

Thomas Ulimwengu, akimtoka beki wa Cameroon.


MSHAMBULIAJI chipukizi na hatari wa Timu ya Taifa ya Vijana, Thomas Ulimwengu anatarajia kutua TP Mazembe kwa mkopo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Wakala wa mchezaji huyo anayetambulika na Fifa, Damas Ndumbaro alisema Ulimwengu atatua Mazembe kwa mkopo ambapo atakaa kwa muda na kisha kutimkia Ufaransa kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye kikosi cha FC Monaco.

"Mazungumzo ya awali bado yanaendelea kati ya kituo cha AFC cha nchini Sweden ambacho ndicho kilikuwa kikimlea mchezaji huyo pamoja na klabu ya TP Mazembe ambao wamepanga kumsajili kwa mkopo,"

"Ulimwengu anatarajiwa kuitumikia Mazembe kwa muda tu kabla ya kuelekea nchini Ufaransa ambapo ndipo anapotarajiwa kwenda kucheza soka la kulipwa endapo atafuzu," alisema Ndumbaro.

Alisema mikakati inaendelea ya kuwatafutia timu za nje ya nchi wachezaji wengine hapa nchini ikiwa na lengo la kuendeleza soka hapa nchini.

Ulimwengu alifanikiwa kufuzu majaribio katika klabu ya Mazembe ambao ni mabingwa wa Afrika mara mbili mfululizo.
 
Niliwafuatilia Ulimwengu na Samatta katika mashindano ya Taifa Cup mwaka jana...wenyewe wakichezea U20 pale DODOMA, Timu yao ikiwa ni waalikwa, hakika ni vijana wazuri.Cha msingi ni kufuata kanuni za soka tu, watafika mbali.
 
Back
Top Bottom