Mshambualiaji shabaha wa Simba- Sc Anaweza Asitue Kutokana na Utata wa Uraia

Baba Kiki

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,544
943
upload_2017-6-14_12-31-50.png




Mshambualiaji wa Timu ya Nkana FC ya Nchini Zambia ambaye pia ni Miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na Mabingwa wa Azam Federation Cup, Simba SC Walter Bwalya amejitokeza na kutoa ufafanuzi kuhusu Uraia wake.

Bwalya ambaye uraia wake Bado unawachanganya wengi Kwa kuwa amezaliwa na Mama Mkongo na Baba Mzambia, amesema wazi wazi kuwa yeye ni Mzambia na Hakuna sababu ya wengine kupinga Jambo hilo.

Suala la Utata wa Uraia wake uliibuliwa na kukomazwa na Klabu ya Dynamos inayoshiriki ligi Kuu Soka nchini Zambia ambao wanadai Mara nyingi Bwalya hubadilisha hata Majina yake ili kuficha uraia wake.

Akizungumza na gazeti la The Times la Zambia ameyataja madai yaliyotolewa na klabu ya Dynamos kuwa ya uzushi na yasio kuwa na msingi.

Zambia

-Sijui ni kitu gani hawa Dynamos wanaongea kuhusu sababu mimi sio Mzambia, Baba yangu ni Mzambia na mama yangu ni Mcongo, hilo linajulikana wazi kabisa", amesema Bwalya.

Mshambuliaji huyo hatari ambaye anatarajiwa kusajiliwa na Simba wakati wowote kuanzia sasa amesema Pia aliwahi kuzichezea Timu za Corboux na Lubumbashi zote za kutoka nchini Congo na kusema kuwa alitumia jina lake la Walter Binene Bwalya na sio Heriter Sawa Kama inavyodaiwa na Klabu ya Dynamos.

Congo

-Nimezichezea Timu hizo lakini sio kwa majina hayo ya Heriter Sawa, niliwahi Pia kuichezea Forest Rangers kama Mzambia", ameongeza Bwalya.

Mshambuliaji huyo ambaye alimaliza Msimu uliopita wa FAZ super Division akiwa na mabao 24 ni miongoni mwa wachezaji wa kigeni ambao wanatarajia kuitwa Simba pamoja na Mganda Emmanuel Okwi hivyo Utata Wa uraia wake unaweza Kukwamisha juhudi za Simba kutaka kumchukua.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zikisema kwamba Aliyefanikisha dili hilo ni Mfanyabiashara Mohamed Dewji 'MO' ambaye ni kipenzi cha mchezaji huyo kwa muda mrefu.


Chanzo: Futaa.com
 
Back
Top Bottom