Acha kudanganya watu wewe Pmaji.
Ngazi ya mshahara wa mwalimu mwenye cheti cha Ualimu Drj IIIA unaanza na TGTS B1, B2 mpaka B10, vivo hivo kwa C, D, na -E10 ambayo E ndio Bar ya mwalimu mwenye ngazi ya cheti ambaye ana haki zote za kufundisha shule ya msingi (akifika hapa kwenye Bar hawezi kwenda F1 mpaka akachukue Diploma ya Ualimu) Kuanzia FI na kuendelea huko mbele ndio Ngazi ya Diploma (kwa Sekondari), Degree, ambapo hapa mwalimu anaweza akawa Afsa Elimu mkaguzi, msaidizi, Mkaguzi mkuu au Afsa Taaluma au cheo chochote chenye ngazi ya Degree, japo ofisi zetu hizi za akina mjomba, hata kama una cheti cha daraja la IIIA (S/Msingi) na ukitaka kuwa Afsa utakuwa Chezea utamu wa Ndugu.
Taarifa hii ni kabla ya waliofika Bar E10 kurukishwa na kupelekwa F1
Kuna baadhi ya walimu wameshapata Barua za Kupandishwa Madaraja.
Ila sasa hapa ndipo kwenye utata:....Wale ambao walikuwa wanapata mapunjo, hawajatumiwa barua lakini kwa wale waliobahatika kupata mshahara kamili, ndio walioletewa barua.
Hivo endelea kuvumilia mpaka Tarehe 20, ukiona hakuna barua inayokuja kwako toka Manispaa..........hapo ndipo uandike barua ya maombi ya kuomba kupandishwa daraja kwa maana ni stahiki yako mkuu Buka Crouch Juniour
Mshahara wa zamani ilikuwa ni Sh 740,890/=...........mshahara mpya ni Sh 945,600/= Mpaka 1,034,990/= (Hapa sasa areas yaani vile vipesa vinavyoweka kila mwezi wa 7 na serikali ndio vinahusika)