Msema kweli ni mpenzi wa mungu hakuna cha kuupiga mwingi ni sifa isiyonauhalisia kwa mheshimiwa raisi.

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Chawa wa ccm na upinzani kwa ujumla wamekuwa wakimuvisha mheshimiwa raisi sifa ambazo hazina msingi huku malalamiko kwa wananchi yakiongozeka mfano mkubwa ni haya yafuatayo-

Unawezaje kumwambia raisi anaupiga mwingi huku bidhaa hazikamatiki kuanzia chakula na bidhaa nyingine

pili unawezaje kumwambia raisi anaupiga mwingi huku malipo ya symbion bilion 353 zimelipwa bila utaratibu na serikali haina majibu kuhusiana na hilo.

Tatu unawezaje kumwambia raisi anaupiga mwingi huku trilion 5 za kodi zilizoamuliwa katika mahakama za rufaa za TRAB TRAT hazionekani zipo wapi

Nne unawezaje kumwambia raisi anaupiga mwingi huku hoja kuhusu trilion 360 hazijajibiwa vizuri na waziri wa fedha ndani ya bunge.


Tano unawezaje kumwambia raisi anaupiga mwingi huku kilio cha umeme nchini kimekuwa tatizo kubwa na serikali haina majibu kuhusiana na tatizo hilo.


Sita unawezaje kumwambia raisi amekopa mikopo hadi kupita kiwango kilichokubaliwa na bunge ambapo trilion 5 hazijuilikani zilipo

Mambo ni mengi mda mchache kimsingi Dr.bashiru hana sababu ya kubezwa kwa kile alichokiongea kwa wakulima na amesema kweli daima sasa nyie vijana mliozoea uchawa mmeona mmushambulie kwa kumuita sukuma gang lakini nawambie kwa sasa mnalamba asali mngejuwa hali ya mtaani ilivyo hivi sasa msingekuwa mnatukana watu wanaosema ukweli kwani ukweli humsaidia raisi na watendaji wake kujirejebisha wanapokosea

Sasa kilichobaki mmebaki wapiga zumali na kutukana wanaomkosoa raisi.

endeleeni.
 
CCM OYEEEEE..!!!!
UCHAGUZI WA CCM. "RUSHWA NJE NJE".

Huo ni uchaguzi jumuia ya vijana CCM mkoa wa simiyu wilaya ya ITILIMA
 
Aupige mwingi kutoka wapi?
Ni dhaifu anavikwa ngao kwa maneno
 
Back
Top Bottom