Kukulia ndani ya CCM siyo hoja ya msingi kosolewa, jirekebishe unapokosea siyo unaupiga mwingi kwa kikundi cha watu wachache

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,620
3,936
Nongwa si kwa ajiri ya kutafta madaraka bali wanahitaji ujirekebishe pale unapokosea tembelea wananchi angalia matatizo waliyonayo hapo utajuwa kama unaupiga mwingi au hamna

Rais Dkt Samia ajue kuwa hao wanaomsifia asifikri kuwa ndio watakaompigia kura bali ni safu yake tu ambayo anaamini kuwa itamsaidia katika uchaguzi mkuu ili aweze kushinda kiti cha uraisi , binafsi ajue kwamba ni vizuri kuwekeza kwa wananchi kwa kuwafanyia kazi kuliko kufrahisha kikundi cha watu wachache akiamini kwamba kitampigania , hao hao wanaomwambia anaupiga mwingi hatiamini watakapofanya tathimini ya ushawishi alionao na kumwambia apumzike.

Dhana ya kuupiga mwingi aliangalie kwa mapana yake maana kwa haya yanayoendelea nchini hasa kipindi hiki ambacho mfumuko wa bei za bidhaa na miradi mingi shule n.k kutokamilika kwa wakati yote haya yatamletea doa kubwa kwenye jamii anayoiongoza.

Kiongozi mzuri ni yule anayefatilia na kusimamia wale anaowaongoza lakini ikitokea tu kila kitu watu wa chini yako waamue wenyewe huenda ukakumbana na fimbo kali kwa wananchi.Hazina kubwa wekeza kwa wananchi mheshimiwa raisi zaidi ya hapo unajidanganya kwa kutegemea kundi hilo.
 
Ma dokta(dr.Bashiru na Dkt:Samia) wanavyotofautiana kihoja na kimtazamo who are you hadi uingilie kati??
Are you a professor?

Kama ww ni degree kushuka chini unajihangaisha tuu cha mhm tunachokiweza kufanya mimi na wewe ni kuwaunga mkono watu wanaodai katiba mpya haijarishi ni vichaa,vilema n.k
 
Maneno haya hayana msingi kwa mwenyekiti wa ccm atambue hao hawatoki leo wala kesho hoja hujibiwa kwa hoja siyo vijembe vya kusema kukulia ndani ya chama! Niupuuzi mtupu maovu yafanyikapo na kufumbia macho kisa tu huwez kuikosoa ccm ukiwa ndani ya ccm
 
Maneno haya hayana msingi kwa mwenyekiti wa ccm atambue hao hawatoki leo wala kesho hoja hujibiwa kwa hoja siyo vijembe vya kusema kukulia ndani ya chama! Niupuuzi mtupu maovu yafanyikapo na kufumbia macho kisa tu huwez kuikosoa ccm ukiwa ndani ya ccmView attachment 2439961
Huyu mama kuna kipindi anaongea kama vile anaongea na wake wenza wake. Kiongozi anakuwa na nongwa na vijembe kama kina Mwijaku.
 
Shida kubwa aliyo nayo Chief Hangaya ni kuto jiamini kuwa ni rais mwenye mamlaka kisheria na kikanuni.

"Kiongozi dhaifu siku zote huwa muoga wa hoja"
 
Back
Top Bottom