Msekwa: Sioni mgogoro UVCCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa: Sioni mgogoro UVCCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr. Zero, Mar 31, 2011.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Msekwa: Sioni mgogoro UVCCM Wednesday, 30 March 2011 21:19 0diggsdigg

  Exuper Kachenje na Ramadhan Semtawa
  WAKATI mpasuko ukionekana kuongezeka ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na viongozi wastaafu, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa ,amesema haoni tatizo lolote.
  Akizungumza kwa simu kutoka jijini Nairobi, Kenya jana, Msekwa alisema wanaoona kuna mgogoro kati ya UVCCM na wastaafu, hayo ni maoni yao.

  “Hayo ni yako, hayo ni yako, hakuna malumbano ndani ya UVCCM na chama. Kwa heri," alisema Msekwa.
  Kauli ya Msekwa imekuja wakati kuna kila dalili ya tofauti za kimtazamo ndani ya UVCCM, kuhusu kauli za Baraza la umoja huo dhidi ya viongozi wastaafu.

  Wakati huohuo, kada wa zamani wa CCM sasa Mbunge Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda, amefananisha malumbano ndani ya chama tawala na maisha ya mbwamwitu porini, ambao kila mmoja hujifuta damu asionekane kama kala mzoga.

  Shibuda alirusha kombora hilo kipindi ambacho CCM imejikuta kwenye malumbano kati ya vigogo wake na UVCCM.
  "Nimekaa CCM miaka 43. Sikuwa napenda iondoke madarakani, lakini sasa lazima Watanzania wafikirie chama mbadala," alisema.

  Shibuda bingwa wa kutumia tamathali za semi kwenye mazungumzo yake, alisema CCM hivi sasa ni sawa na pori la mbwamwitu ambalo kila mmoja hujaribu kujipangusa damu ili asijulikane madhambi yake.
  Alifafanua kwamba vijana wa chama hicho, nao wamekuwa vibaraka wa makundi kwa kutaka maisha bora na kusahau mbele watakuwa watwana zaidi.

  "CCM ya sasa haimtetei mnyonge, vijana ambao wakati wa Tanu walikuwa na msimamo madhubuti kulinda maslahi ya taifa sasa wanashiriki kurejesha utwana kwa kuwa vibaraka wa makundi ya kisiasa," alisisitiza.

  Mbunge huyo alisema umefika wakati Watanzania wanapaswa kutambua vyama vya siasa ambavyo ni Saccos na kampuni, vinavyofanya siasa kutafuta ruzuku na vile vinavyotetea maslahi ya jamii.

  Shibuda alisema hali ilivyo sasa malumbano ndani ya CCM inaonyesha sehemu kubwa ni watu wanaopigania maslahi binafsi na kusahau wananchi.

  Katika kuonyesha msisitizo, Shibuda aliweka bayana kwamba kutokana na malumbano hayo kati ya wazee na vijana, imeonyesha jinsi CCM ilivyotoka kwenye misingi yake iliyorithi kutoka Tanu, ndio maana rasilimali za nchi zinaporwa wao wanazozana.

  Akijivunia rekodi yake ya ukada wa CCM tangu Tanu kwa miaka 43, Shibuda aliponda utaratibu wa vikao kushughulikia matatizo na watu wachafu ndani ya chama, kwani havina tija.

  "Mimi nimekaa ndani ya CCM kwa miaka 43, mambo ya vikao nikupoteza muda tu. Ndio maana niliapa kutopeleka tatizo langu kwenye kikao chochote, kwani haviwezi kutenda haki," alisisiiza Shibuda.
   
Loading...