Msekwa: CCM imejiandaa kushindwa

Msekwa: CCM imejiandaa kushindwa

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Aliyekuwa Makamu M/kiti wa CCM na Spika mstaafu Pius Msekwa amesema Chama cha Mapinduzi kimejiandaa kwa yote kushinda au kushindwa kwa vile hakitakuwa chama cha kwanza barani Afrika kushindwa.

Ameongeza kuwa CCM isibweteke kwa kuwa ni chama kikongwe, amesema kuna vyama vilivyopigania uhuru kama KANU na vingine vilijikuta vikiangushwa na vyama vidogo na vichanga kwa kusimamisha wagombea wasiokubalika.

Chanzo: Mtanzania.
 
Aliyekuwa Makamu M/kiri wa CCM na Spika mstaafu Pius Msekwa amesema Chama cha Mapinduzi kimejiandaa kwa yote kushinda au kushindwa kwa vile hakitakuwa chama cha kwanza barani Afrika kushindwa.

Ameongeza kuwa CCM isibweteke kwa kuwa ni chama kikongwe, amesema kuna vyama vilivyopigania uhuru kama KANU na vingine vilijikuta vikiangushwa na vyama vidogo na vichanga kwa kusimamisha wagombea wasiokubalika.

Chanzo: Mtanzania.
Hii mada nilidhani kaandika mtu wa maana kumbe wewe hewa! Hovyo kabisa.
 
Aliyekuwa Makamu M/kiti wa CCM na Spika mstaafu Pius Msekwa amesema Chama cha Mapinduzi kimejiandaa kwa yote kushinda au kushindwa kwa vile hakitakuwa chama cha kwanza barani Afrika kushindwa.

Ameongeza kuwa CCM isibweteke kwa kuwa ni chama kikongwe, amesema kuna vyama vilivyopigania uhuru kama KANU na vingine vilijikuta vikiangushwa na vyama vidogo na vichanga kwa kusimamisha wagombea wasiokubalika.

Chanzo: Mtanzania.

Ni kweli katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, pia naona wapinzani wamejiandaa vema katika uchaguzi wa mwaka huu 2015.
 
Mzee kaona mbali. Ccm Tutakiweka makumbusho ya taifa. Hata wajukuu wetu watakuja kushangaa jinsi ccm ilivyo tutawala mda mrefu. R.I.P ccm
 
wenye hekima wameshaliona hilo, hata Kikwete ana kwenye kutoa nishani alikuwa mwenye sura ya uzuni sana
 
Hii mada nilidhani kaandika mtu wa maana kumbe wewe hewa! Hovyo kabisa.
Hii habari imeripotiwa katika gazeti la Mtanzania ukurasa wa mbele kabisa na kichwa cha habari kinasomeka: "Msekwa:CCM inaweza kushindwa".
 
Mtanzania sio gazeti la kuamini n gazeti la pro lowasa
 
Msekwa...ndio mmoja wapo aliyehusika kumkata Lowassa...

Sasa anaisoma number...UKAWA + Lowassa = CCM kifo cha kibaka....

Hakuna namna CCM itapona, UKAWA + Lowassa wakitia timu, huyu mzee kanafiki sana haka, ndio watu wanaohusika kuua CCM, shit kabisa..
 
Unaota ndoto za mchana wewe
CCM ni taasisi sio sacoss mwisho wa lowasa na siasa zenu za kinafiki zitafikia oktoba 25
 
Hivi gazeti likiripoti alichokisema mtu na lingine likakiacha, hili lililoripoti unalichukia?

Fahamu kwanza historia ya magazeti na yanaripoti kuhusu nani au nini?
 
Ameshaona upepo unapovuma.
Na mgombea urais kupitia ukawa akishajulikana huyo magufuli hatakuwa na hali.
 
Du ameona mbali kwa kutumia uzoefu na wanapoongea wazee kama hawa ujue mambo makubwa yanakuja. Wasioona mbali kama bwana mdogo Nape watabaki kujifariji. Pity on him!!!!
 
Back
Top Bottom