Msekwa alia na gharama za uchaguzi Tarime | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa alia na gharama za uchaguzi Tarime

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Absolute, Oct 23, 2008.

 1. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2008
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Pius Msekwa, amesikitishwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumiwa na chama chake; Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na serikali katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni katika Jimbo la Tarime.

  Msekwa, aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamuri ya Muungano, alieleza masikitiko yake kwenye mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) juzi, katika kipindi cha ‘Dira ya Dunia’, lakini alikataa kutaja kiasi cha fedha kilichotumiwa na kila chama pamoja na Serikali.

  Katika kampeni za uchaguzi huo, kulikuwa na ushindani mkubwa kwa vyama vya CCM na CHADEMA, vilivyoshindana kwa kutumia helikopta kwa lengo la kusaka wapiga kura na kufanya mikutano mingi zaidi kwa siku.

  Gharama zilizotumika na vyama hivyo ni kubwa mno kuliko hata kile kilichokuwa kikitafutwa. Pamoja na kuainisha udhaifu huo, Msekwa alikataa kutaja gharama ambazo chama chake kilitumia, lakini alisisitiza kuwa gharama hizo hazilingati na kile kinachotafutwa wakati wa kampeni.

  “Sijui kiasi gani kilichotumika...ila ninachojua ni kwamba fedha nyingi zimetumika…bila kujali kama chama kimeshinda ama hakikushinda na huwezi kuzithaminisha na kile kilichopatikana,” alisema Msekwa.

  Aliulaumu mfumo wa uchaguzi nchini kuwa ndiyo sababu ya kampeni kutumia gharama kubwa zaidi, ambazo alisisitiza kuwa hazina msingi na kushauri mfumo huo ubadilishwe ili kunusuru taifa kuingia katika matumizi yasiyo ya lazima.

  Msekwa alisema gharama za uchaguzi hazikwepeki katika uchaguzi mkuu, lakini kwenye uchaguzi wa marudio zinaweza kukwepeka kupitia mfumo wa uwiano wa uwakilishi, ambao umeshaanza kutumika katika nchi kadhaa barani Afrika, zikiwamo Afrika Kusini na Msumbuji.

  “Lazima tubadili mfumo na katika mfumo huo utakaobadilishwa tushindanishe vyama na si wagombea katika chama, tukifuata mfumo huo, viti vya bunge vitapatikana kutokana na uwiano wa kura ambazo chama husika kimepata. Jambo hilo baadaye huepusha kuwapo kwa chaguzi ndogo kwani chama chenye uwiano mkubwa moja kwa moja humtoa mrithi wa nafasi iliyoachwa wazi,” alisema Msekwa.

  Katika uchaguzi mdogo wa Tarime uliofanyika Oktoba 12 kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Chacha Wangwe (CHADEMA), CCM inadaiwa kutumia zaidi ya sh bilioni moja.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hadi hivi sasa haijatoa gharama halisi za uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa vyama vya siasa nchini.

  Source"Tz Daima"

  My question is"CCM ingeshinda angekuwa na ujasiri wa ku-lament as above?"
   
 2. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Lakini anatakiwa awe makini maana hata idea ya kupigia kura chama CCM imewakalia vibaya! Anaamini wanaweza kushinda na hii CCM ya Chama cha Mafisadi! Msekwa apumzike, hiyo tafakakuri yake ingekuwa na maana sana kama angeitoa akiwa mstaafu wa siasa! Mbona hashauri rais wa nchi asiwe mwenyekiti wa chama ili asije akaamrisha majeshi (polisi nk) kusaidia chama chake kushinda! Huyu ni mnafiki tu!
   
Loading...