Msanii Juma Kilowoko (SAJUKI) amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.
Sajuki ambaye ameacha mjane ambaye pia ni msanii aitwaye Wastara ambaye ni mlemavu wa mguu mmoja ambao ulisababishwa kwa kupata ajali mnamo mwaka 2008 siku chache kabla ya ndoa. Hata hivyo Sajuki aliamua kumuoa hivyo hivyo kwani alikuwa ameshapeleka posa kwa kina Wastara.
Tukio hilo liligusa hisia za watu wengi na kumchukulia Sajuki kama shujaa na mwanaume mwenye mapenzi ya kweli kwa kitendo hicho alichokifanya.
Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua muda mrefu yalipamba moto
Hata hivyo alikuwa hajapona sawa sawa na alikuwa anajiandaa kurudi tena India kwa matibabu zaidi.. na hii alikiri kwenye kipindi cha 'Mkasi' kinachoendeshwa na kituo cha televisheni cha EATV.
Sajuki ambaye ni mngoni ameshacheza maigizo na filamu na wasanii wengi karibia wote wenye majina hapa Tanzania.
Sajuki kwa kusaidiana na mkewe walifungua kampuni ya productions kwa ajili ya filamu (movies) za hapa hapa nchini.
nipo hapa nyumbani naskiliza radio na mtanagazaji anatangaza kuwa muigizaji wa siku nyingi sajuki amefariki dunia leo asubuhi kutokana naradhari yaliyokua yanamsumbua.amefarikia katika hospital ya muhimbili.
chanzo ni radio 88.5 fm
Msanii wa bongo movie ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda sasa, amafariki dunia katika hospital ya taifa ya muhimbili. R.I.P Sajuki
Source: power breakfast - clouds fm