*Msanii na maskini*

*Msanii na maskini*

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,638
Image may contain: one or more people



Palikuwa na mchoraji katika mji mmoja. Mchoraji huyo alikuwa na umri wa utu uzima.

Alikuwa akichora picha nzuri na akiziuza kwa bei kubwa sana.

Siku moja wakamjia maskini na mafukara wa mji ule wakamwambia:

"Wewe unatengeneza kipato kikubwa sana kwa kazi yako hii, kwanini hutaki kutusaidia sisi watu wa hali ya chini?

Watazame wenzako wauza nyama; ijapokuwa hawana kipato kikubwa kila siku hutoa vipande vya nyama kutusaidia tusiojiweza."

Mchoraji hakuwajibu chochote ila aliwaonyeshea uso wa furaha tu.

Wale mafukara wa mji ule waliondoka wakichukizwa na tabia ya yule mchoraji.

Ikawa wakitangaziana pale mjini kuwa mchoraji yule Mwenyezi Mungu amemjaalia kipato lakini ni mbahili na hawasaidii wasiojiweza.

Baada ya muda mchoraji yule alianza kuugua. Hakuna mwanakijiji yeyote aliyekwenda kumuona mpka akafa.

Baada ya kufa yule mchoraji siku zilipita na ikawa wale wauza nyama hawatoi tena nyama kwa ajili ya kuwasaidia wasiojiweza.

Wale mafukara ikabidi wawaulize wauza nyama ni kwanini hawawasaidii tena nyama kama zamani.

Wauza nyama wakawajibu kuwa yule mchoraji aliyekufa alikuwa akiwapa pesa kila mwezi kwa ajili ya kuwanunulia nyama wasiojiweza, akiwaagiza wawape bure kila siku. Alipofariki likasimama jambo hilo kwani hazikutoka tena pesa za kuwanunulia wao nyama kwa kuwa mchoraji ameshakufa. . .
 
Jah bless....



CCM OYEEE....KIDUMU CHAMA CHA MAPUNDUZI....
 
Back
Top Bottom