Jifunze kisa hiki Cha kusisimua!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,726
5,475
Palikuwa na mchoraji mmoja katika moja ya mji mchoraji huyo alikuwa mwenye umri wa utu uzima.

Alikuwa akichora picha nzuri sana na akiziuza kwa gharama kubwa sana.

Siku moja wakamjia maskini na mafukara wa katika mji ule wakamwambia.

"Wewe unatengeneza kipato kikubwa sana kwa kazi yako hii ni kwanini hutaki kutusaidia sisi watu wa hali ya chini?

Watazame wenzako wanaouza nyama ijapokuwa hawana kipato kikubwa lakini kila siku hutoa vipande vya nyama kuwasaidia wasiojiweza."

Mchoraji hakuwajibu chochote ila aliwaonyeshea uso wa furaha tu.

Wale mafukara wa mji ule waliondoka wakichukizwa na suala lile la mchoraji.

Ikawa wakitangaziana pale kijijini kuwa mchoraji yule M/ Mungu amemjaalia kipato lakini ni mbahiri si mwenye kuwasaidia wasiojiweza.

Baada ya muda mchoraji yule alianza kuugua lakini hakuna mwanakijiji yeyote aliye kwenda kumuona mpaka akafa.

Baada ya kufa yule mchoraji siku zilipita na ikawa wale wauza nyama hawatoi tena nyama kwa ajili ya kuwasaidia wasiojiweza.

Wale wanakijiji ikabidi wawaulize wale wauza nyama ni kwanini hawawasaidii tena nyama kama zamani?

Wauza nyama wakawajibu kuwa mchoraji alikuwa akiwapa pesa kila mwezi kwa niaba ya kuwanunulia nyama wasiojiweza.

Na wawape bure kila siku lakini alipofariki likasimama jambo hilo kwani hazikutoka tena pesa za kuwanunulia wao nyama kwa kuwa mchoraji ameshakufa.

Baadhi ya watu huwenda wakawa wanakudhania vibaya lakini na wengine huenda wakakuona msafi kama maji yasiyoharibiwa.

Tambua hawakuzidishii kitu kwa wao kukuona ww kuwa ni msafi

Na wala hawakupunguzii kitu kwa wao kukudhania vibaya.

Kilichomuhimu ni vile akujuavyo mola wako kuwa ww ni mtu wa aina gani kwani yy ndiye anaejua ya siri na ya dhahiri.

Usimuhukumu mtu yeyote kwa muonekano wake wa nje kwani hujui undani wake.

Kwani hujui undani wake kuna baadhi ya matendo ayafanyayo lau kama ungeliyajua ungemuhishimu sana.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom