MAFISADI Tanzania walianza tangu siku ile Mwinyi alipotangaza OPEN MARKET, maana hata mbwa alianzisha business na kununua shea mabalimbali katika makampuni mbalimbali. Matokeo yake, nani atamfunga mwenzie, mahakama ni mafisadi, polisi ni mafisadi. Nchi nzima imejaa mafisadi, toka rais hadi wafagia barabara.
Suala la kuwasamehe halitoshi. Kama kuna mtu mwenye uwezo na busara, hizo pesa walizowekesha nchi za nje ziwe frozen kama walivyomfanyia Malima na vijisenti vyake alivyokuwa amewekeza Uingereza, matokeo yake alipokwenda huko ili atumia, mwanae akamwambia "baba hela zimezuliwa", akazirai na kufariki.
Wakati umefika wa kuirudishia Tanzania TAIFA lake, TAIFA limekufa tangu siku ile Mwinyi atangaze, iliyobaki ni NCHI tu. najua Rais Kikwete hawezi kufanya lolote maana naye ana chake somewhere, isitoshe hawa MAFISADI wana uwezo mkubwa kwa kutumia hizo pesa za kuweka mawakili shujaa, kiasi kwamba Rais anaogopa kuwafungulia mashitaka maana itaigharimu serikalo pesa nyingi sana, na hasa ukizingatia kuwa Wafadhili wameanza kushtuka kutoa misaada kwa vile tunakula tu bila kujali kujenga Taifa.
Watanzania wakati wa vitendo umefika, tuache kuogopana tuseme ukweli na ikiwezekana hawa mafisadi ambao tuna ushahidi nao wafikishwe mbele ya sheria siyo kuunda tume ya kuwachunguza na kuwapeleleza na kuandika makaratasi chungu nzima, then hamna kinachofanyika.
Watafutwe Polisi waaminifu na Mahakimu waaminifu, kesi zifunguliwe na ziendeshwe KISHERIA, kam haiwezekani, basi zipelekwe kwenye BARAZA la kimataifa kama Rais anaogopa kuwashtaki wakati anajua wana pesa zetu na bado wanatamba.
WAKATI NI HUU TUSINGOJE KESHO.