Msajili wa Hazina agoma Shirika la UDA kuchukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Msajili wa Hazina Agoma Shirika la UDA Kuchukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam



MSAJILI wa Hazina ametupilia mbali maombi ya Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam ya kutaka kurudishiwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) kwa kusisitiza kuwa Kampuni ya Simon Group ina hisa halali katika shirika hilo.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaac Mwita, alikaririwa na vyombo vya habari jana akimtaka Msajili kukadhibidhi shirika hilo kwa uongozi wa Jiji kwa madai kuwa Simon Group walinununua shirika hilo kinyume cha taratibu.

Msajili alisema pia serikali haina mpango wa kuuza hisa zake za asilimia 49 inazomiliki katika shirika hilo.

Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam waliomba wapewe hisa hizo za serikali ikiwa hawatarudishiwa hisa za Simon Group.

Mkuu wa Kitengo cha Habari wa ofisi ya Msajili wa Hazina, Gerard Chami, jana alisema kuwa ofisi yake haiwezi kubadilisha mkataba wa umiliki wa Uda.

“Msajili anakamata hisa za serikali ambazo ni mali ya Watanzania, hazihusiani kwa namna yoyote na hisa asilimia 51 za Jiji ambazo walishaziuza kwa kampuni ya Simon Group. Tunashangaa wanapotaka tuingilie mambo yao ambayo kimsingi hatuhusiki,” alisema Chami.

Chami alieleza kuwa kulikuwa na kesi iliyokuwa mahakamani baina ya Jiji na kampuni ya Simon Group Ltd. Iliamuliwa Simon Group ilipe Sh. bilioni 5.5 ili kununua hisa za Jiji na alifanya hivyo na kwa mazingira hayo, Msajili hadi sasa anamtambua kama mwanahisa mwenza wa Uda.

Alifafanua kuwa hakuna namna ambayo Msajili atajihusisha na hisa hizo kwa kuwa siyo wajibu wake bali anachotakiwa ni kumtambua mwanahisa mwenzake ambaye kwa sasa ni kampuni ya Simon Group.

“Suala hili linachukuliwa kisiasa zaidi, lakini ukweli unajulikana kwani ni sawa mtu alikuwa na mali yake akaamua kugawa sehemu na kumpa mwingine aliyehitaji kwa wakati huo, lakini kwa sababu zake kile alichogawiwa akaamua kuuza kwa mtu mwingine, ni vigumu kurudi kwa sasa kumweleza aliyegawa awali kugawa tena hisa zake," alifafanua.

“Yeyote aliyeuziwa hisa hizo sisi tunamtambua ndiye mwanahisa mwenza, tunachojua kwa sasa kampuni ya Simon Group ndiye mwanahisa mwenza kwa kuwa alishamaliza kulipa kwa kutekeleza amri ya mahakama,”
alisema.

Alibainisha kuwa hisa asilimia 49 za serikali ina hiari nazo kama ni kuuza kwa faida au kwa ajili ya kupeleka fedha katika eneo jingine lenye maslahi ya jamii na siyo kwa Jiji linavyotaka kumpa mwanahisa mwenza katika shirika hilo.

Meya Mwita alisema juzi kuwa Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam liliazimia katika kikao chake kuwa fedha zaidi ya Sh. bilioni 5.5 zilizolipwa kwa Jiji na kampuni ya Simon Group kwa ajili ya kununuliwa hisa zisirudishwe hadi tathmini ya kina itakapofanyika na kujiridhisha kuwa hadaiwi chochote kwa kutumia mali mbalimbali za Uda kwa maslahi yake.

Pia waliunda kamati ndogo ya wajumbe watatu ambao ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea na Mwanasheria wa Jiji, Jumanne Mtinangi kwa ajili ya kufuatilia suala hilo.

Naye Ofisa Habari wa Simon Group, Deus Buganywa, alisema jana hawajapokea barua yoyote kuhusiana na kutakiwa kurejesha hisa hizo baada ya kuulizwa juu ya sakata hilo la Uda.

Nawasilisha
 
Mi nawashangaa wanapeleka vitu kisaisa zaidi, maana sidhani kama walikua hawajui kua msajili hana mamlaka ya kutengua maamuzi ya awali ya Jiji.. kama ishu ni kua hisa hizo hazikuuzwa kihalali basi watumie njia zinazofaa kupinga uuzwaji huo wa Hisa. hapa naona kabisa kuna kutwanga maji kwenye kinu kupeleka ishu kisiasa zaidi
 
Hii ni ishu ya udanganyifu...kisheria ni lazima ichunguzwe. Na uchunguzi utabatilisha au kuridhia kilichotokea. Tusubiri...hata hivyo ni lazima umma wa watanzania waelewe msajili wa hazina ni mteule wa JK ...na pia uuzaji wa UDA unahusisha familia ya JK na CCM. Hili ndilo kundi hatari sana linalopinga harakati za JPM na hakika msajili huyu ni vigumu kutetea maslahi ya Umma. Paul Makonda pia ni swahibu wa familia hii...sijui atajiepusha vipi na jambo hili. Ningependa kuona uchunguzi utafikia wapi na taarifa yake itatumika vipi..hakika uuzwaji wa Uda ni utapeli na ndiyo maana kila mara na mpaka leo umekuwa ukilalamikiwa. Kuna kila sababu kwa serikali ya JPM kuepuka kadhia ya kinyesi hiki ili kujiepusha na harufu hii iliyoachwa na JK na familia yake.

Napendekeza pia msajili huyu aondolewe au ajiunge na wananchi ili wachache waache kuwanyonya watu wengi!
NI MAONI YANGU TUU..INAWEZEKANA HAYATAAWAFURAHISHA WANAOISHI KAMA MALAIKA
 
Hii ni ishu ya udanganyifu...kisheria ni lazima ichunguzwe. Na uchunguzi utabatilisha au kuridhia kilichotokea. Tusubiri...hata hivyo ni lazima umma wa watanzania waelewe msajili wa hazina ni mteule wa JK ...na pia uuzaji wa UDA unahusisha familia ya JK na CCM. Hili ndilo kundi hatari sana linalopinga harakati za JPM na hakika msajili huyu ni vigumu kutetea maslahi ya Umma. Paul Makonda pia ni swahibu wa familia hii...sijui atajiepusha vipi na jambo hili. Ningependa kuona uchunguzi utafikia wapi na taarifa yake itatumika vipi..hakika uuzwaji wa Uda ni utapeli na ndiyo maana kila mara na mpaka leo umekuwa ukilalamikiwa. Kuna kila sababu kwa serikali ya JPM kuepuka kadhia ya kinyesi hiki ili kujiepusha na harufu hii iliyoachwa na JK na familia yake.

Napendekeza pia msajili huyu aondolewe au ajiunge na wananchi ili wachache waache kuwanyonya watu wengi!
NI MAONI YANGU TUU..INAWEZEKANA HAYATAAWAFURAHISHA WANAOISHI KAMA MALAIKA
Vipi mamlaka ya Msajili ynamuezesha kubatilisha kile kilichofanyika? au inatakiwa jiji wapeleke ishu za kisheria ili zimuezeshe kubatilisha? kama hana mamlaka hayo basi watu wataendelea kucheza sindimba tu
 
Ukiuziwa ng'ombe ukapewa na receipt ya manunuzi, ikiwa aliyekuuzia huyo ng'ombe hakuwa na uhalali wa kumuuza ng'ombe huyo basi akitokea mtu akathibitisha pasipo shaka kuwa aliyepaswa kuuza ng'ombe siye aliyeuza, basi umiliki wa ng'ombe unakuwa batili kwa aliyemnunua!!

Sana sana atatakiwa akamalizane kiutu uzima na aliyemuuzia.

Simon group wameliwa, wasubiri muda.

Kukataa kwa msajili ni sawa na kataa ya mtongozwaji, hatimaye mambo huwa.
 
madiwani wanasema hakuipita kwenye utaratibu wa uuzwaji na msajili anatetea uuzwaji yeye ana maslahi gani,na je uda ilikuwa na thamani ya bilion 5.5tu,yaani yadi, majengo,mabasi,ni kiasi cha bilion 5.5.hapo inaonekana shida ipo.vp kuhusu hela za kuuzwa kuingia kwenye account ya mtu binafsi.??
 
Hii ni ishu ya udanganyifu...kisheria ni lazima ichunguzwe. Na uchunguzi utabatilisha au kuridhia kilichotokea. Tusubiri...hata hivyo ni lazima umma wa watanzania waelewe msajili wa hazina ni mteule wa JK ...na pia uuzaji wa UDA unahusisha familia ya JK na CCM.

Hili ndilo kundi hatari sana linalopinga harakati za JPM na hakika msajili huyu ni vigumu kutetea maslahi ya Umma. Paul Makonda pia ni swahibu wa familia hii...sijui atajiepusha vipi na jambo hili.

Ningependa kuona uchunguzi utafikia wapi na taarifa yake itatumika vipi..hakika uuzwaji wa Uda ni utapeli na ndiyo maana kila mara na mpaka leo umekuwa ukilalamikiwa.

Kuna kila sababu kwa serikali ya JPM kuepuka kadhia ya kinyesi hiki ili kujiepusha na harufu hii iliyoachwa na JK na familia yake.

Napendekeza pia msajili huyu aondolewe au ajiunge na wananchi ili wachache waache kuwanyonya watu wengi!
NI MAONI YANGU TUU..INAWEZEKANA HAYATAAWAFURAHISHA WANAOISHI KAMA MALAIKA

Ndugu yangu hata watu wangelia machozi ya damu mwisho wa kilio/vilio ni sheria na taratibu zilifuatwa?Siku zote tunasema mtaji wa ccm na waliopo madarakani ni umbumbumbu,shida/umaikini na kukosa elimu kwa wengi wa watanzania.Hisa za jiji zilizwa kwa aliezinunua kwa bei waliotaka wasimamizi wa wananchi(madiwani na wabunge)waliokuwepo wakati huo wakiongozwa na msomi mkubwa Didas Masaburi.Sina uhakika wa elimu za hao wajumbe waliopitisha na kuridhia hisa kuuzwa kwa wakati huo ila sidhani kama alikuwepo aliezidi darasa la saba na form four kwa waliokuwa wabunge.Kama alikuwepo aliekuwa na degree hatujui kama tusivyojua walichopewa katika ushawishi huo.Ninachoelewa ni kuwa walikuwa wafia chama chao cha mbele kwa mbele na kuzisoma namba.Kilichokuwa muhimu hadi sasa bado ni muhimu ni sheria za uuzwaji na umiliki kufuatwa.Kudhihirisha hilo ndio maana hata kesi mahakamani mnunuzi wa hisa alishinda.Sasa kumwambia msajili awauzie hisa za serikali mtasubiri aagizwe na serikali kuziuza vinginevyo hana mamlaka hiyo.Kuihusisha familia ya Kikwete katika sakata hili inakubidi uende kwanza brela kujua wamiliki wa hizo hisa ukilikosa jina urudi kuiomba familia radhi.Pia kuwaaminisha wasomaji na wananchi kuwa familia hii inapiga vita juhudi za raisi wa sasa ni suala la ushahidi mzito usiouweza linapokuja suala la mahakama.Ndio JK au uongozi wake ulimwajiri huyu msajili kutokana na sifa zake ila haumfundishi jinsi ya kutenda kazi zake na kudhani Makonda wala waziri mkuu watavunja sheria kuwatetea wananchi sahau.SIASA NA SHERIA NI VITU VISIVYOTEGEMEANA KAMWE.NIWEKE UPENDAKO WALA MIMI SIO WA KUNDI UTAKALONIWEKA.
 
Msajili wa Hazina Agoma Shirika la UDA Kuchukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam



“Msajili anakamata hisa za serikali ambazo ni mali ya Watanzania, hazihusiani kwa namna yoyote na hisa asilimia 51 za Jiji ambazo walishaziuza kwa kampuni ya Simon Group. Tunashangaa wanapotaka tuingilie mambo yao ambayo kimsingi hatuhusiki,” alisema Chami.



Nawasilisha


Msajili yupo sahihi, HISA zilizouzwa ni za JIJI na sio za SEREKALi so hamuhusu, JIJI wajipange waende mahakamni wakadai mali yao zaidi ya hapo hakuna jingine tumeliwa!
 
Jiji linatakiwa kudhibiti mali zake kwa nguvu, aliyejimilikisha bila uhalali aende mahakamani, hapo kesi itaanza na haki kutolewa.
Kuanza kuomba kurudishiwa kunamaanisha kuwa jiji linayafahamu na kuyakubali mauzo hayo.
 
Back
Top Bottom