Msafara wa Naibu Waziri Jafo wapotea

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
upload_2016-4-21_14-11-10.png


Msafara wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo leo asubuhi ulipotea njia kutokana na watumishi wa Manispaa ya Dodoma kutojua eneo ambalo waziri huyo alikuwa analitembelea.

Waziri Jafo alikuwa amepanga kufanya ziara kwenye Shule ya Msingi ya Nzuguni B kwa lengo la kuangalia mapungufu, hasa tatizo la uhaba wa madawati, lakini hakufika kama alivyotarajia kutokana na watumishi hao kutojua eneo ambalo shule hiyo iko.

Shule hiyo haijawahi kutembelewa na ofisa elimu tangu mwaka 2007 licha ya kuwa kilomita 6 kutoka katikati ya mji.

Naibu Waziri alikasirishwa na kitendo hicho akawataka watumishi wa idara ya Elimu wajipime kama wanastahili kuendelea kufanya kazi.

“Mstahiki Meya, mimi niliona wazi kuwa watumishi wako wananipoteza," alisema Waziri Jafo.

"Nimechukia sana na hawa watu. Tatizo lao ni kwamba hawajawahi kuja katika shule hii tangu mwaka 2007, lakini wamekaa ofisini tu. Ikiwezekana waondolewe na kupelekwa vijijini,” alisema Jafo.

Chanzo:Mwananchi
 
“Mstahiki Meya, mimi niliona wazi kuwa watumishi wako wananipoteza," alisema Waziri Jafo.

"Nimechukia sana na hawa watu. Tatizo lao ni kwamba hawajawahi kuja katika shule hii tangu mwaka 2007, lakini wamekaa ofisini tu. Ikiwezekana waondolewe na kupelekwa vijijini,” alisema Jafo.

Kumbe mtumishi kupelekwa kijijini ni adhabu!!!!!
 
Kwa hiyo vijijini ni sehemu ya wahalifu, huyu waziri ameanza kulewa madaraka, atuombe radhi haraka sana watu wa vijijini
 
Jafo naye kama waziri amechemka kufikiri vijijini ndiko wanapaswa kwenda watu anaowaona hawafai. Watu wa vijijini mnawazarau sana nyie maboss, ndio maana wakiwapa kura hamrudi tena kuwaona, ukikaribia uchaguzi mnajifanya kwenda T-shirt za kugawa.
 
Huenda kura ya mtu wa mjini zinahesabika mbili, wakijijini zinahesabika nusu. Dah hii ni dharau kwa utu wa mwanadamu
 
Huyu Jafo huko Kisarawe kwake kuna shule zina miaka zaidi ya 15 sio tu hazijatembelewa lakini huko kitachokujulisha kwamba umefika shule ni sare za shule tu
 
mawaziri Awamu hii wanapiga jaramba ndani tu! Hakuna mambo ya kuruka ruka na kanyonyi, kwenda kutumbua maraa nje ya nchi haaaaaaaaaaaaa.

Maana enzi za mzee jakaya, mawaziri walikua wanapishanatu Angani, Ahaaaaaaaaaaaaaaaa, kwisha Habari yao BG Up Brother Magu, safi sana Mkuu.
 
Back
Top Bottom