Msaada

KISUNZU YP

Senior Member
Jul 30, 2016
114
37
Wadau wa JF habari naomba mchango wa mawazo namna ya kufanya.
Mimi ni mtumishi katika kada ya Afya nimeajiriwa katika mkoa wa Tabora kwa Mkurugenzi mtendaji Wilaya ya Sikonge mwaka 2015 mwezi wa nne Kama Tabibu Msaidizi daraja la II(Clinical Assistant II).

Kabla sijamaliza chuo nilipungukiwa ada ya masomo nikaenda kusaini mkataba Halmashauri ya Wilaya Kigoma kwa masharti kwamba nitakapomaliza gu nitalazimika kuajiriwa na serikalini katika wilaya hiyo tena nitafanya kazi miaka 5 ndani ya Wilaya hiyo bila kuhama Kwamba Halmashauri itapeleka taarifa kwenye mamlaka za Ajira.

Ili ajira yangu itokee hapo,bahati mbaya tukamaliza ajira zikatoka wakati hawajafanya hivyo ikatokea wilaya ya Sikonge huku niliko sasa ajira ilitoka mwezi wa kwanza January nikaambiwa usiende kuripoti Sikonge tunaenda wizarani ili Wakubadilishie nikakaa toka Januari,Februari na machi nikaona huu ni ujinga nitakosa ajira kote maana mwisho wa kuripoti ulishaisha huku haijabadilika.

Mwezi wa nne nikaondoka kurepoti hapa nilipo sasa Sikonge nimepata tu barua ya ajira nikatumiwa SMS kuwa post imebadilika sasa ni Kigoma huku nilishajaza taarifa zangu Sikonge Kigoma wakaniambia uje na huku tukufungulie File ili tushindane nao wa Sikonge mimi nikaogopa mambo ya Mbeleni.

Sasa mwaka jana nikaandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma kupitia kwa Mkururugenzi wangu wa Sasa (Sikonge) anipe utaratibu wa kwenda kutimiza mkataba Wangu na Yeye lakini Nilijibiwa na Mkurugenzi wangu wa sasa kwa barua kuwa Kuhama mpaka miaka 3 tena kwa kubadilishana.

Naombeni ushauri mimi nataka kurudi(kuhama) kwetu kigoma huku sijakukubali sana nianzie wapi nifate kipi kwa sababu hiyo ili nipate transfer? Na nakala ya mkataba bado ninayo.


Asanteni
 
Naombeni ushauri mimi nataka kurudi(kuhama) kwetu kigoma huku sijakukubali sana
Nilichaguliwa shule fulani hivi ipo mbali na mkoa niliozaliwa na mbali na mkoa niliokulia, tulipofika mkuu wa shule akasema "Wengi mmeletwa hapa hamkuichagua hii shule na nina uhakika wengine hamjawahi kuisikia. Lakini nyinyi kuletwa huku siyo makosa, ni katika harakati za kujenga umoja, mshkamano na kuua ukabila miongoni mwa waTanzania."
Maneno yalinigusa nikadhamiria kubaki nimalizie elimu yangu kule, nikahama baada ya kuona serikali haipeleki mahitaji ya msingi ya kielimu kwa shule kama zile.
nianzie wapi nifate kipi kwa sababu hiyo ili nipate transfer? Na nakala ya mkataba bado ninayo.
Asanteni
Malizia hiyo miaka 3 ndiyo uufanye huo mpango kama ulivyojibiwa au unaweza kutoka kabla ya muda huo?
 
Back
Top Bottom