Kheri ya mwaka mpya 2015. Natumaini weekend inaenda vizuri kabisa.
Wadau wa jukwaa hili kama kichwa cha habari kinavyosema najitokeza kwenu kuomba msaada wenu.
Mimi ni binti wa kati ya miaka 27-29, nina degree ya computer science, baada ya kutafuta kazi kwa mda mrefu bila mafanikio na sasa nimechoka kukaa tu natafuta kazi yoyote halali itakayoniingizia kipato mkoa wowote nipo tayari, kwasasa ninaishi Dar es Salaam.
Mdau anaeweza kunisaidia kutoka katika janga hili hata kwa mawazo tu tuwasiliane kwa pm. Natanguliza shukrani zangu za dhati.