Msaada wakuu kwa graduate huyu

Msaada wakuu kwa graduate huyu

NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
333
Reaction score
90
Habari wakuu, Mimi ni graduate ninaeendelea kusaka ajira. Katika kipindi hiki cha utafutaji wa ajira nimekuwa sina kazi yoyote ya kuniingizia kipato chochote cha kupata pesa kidogo kwa ajili ya matumizi yangu ikiwa ni pamoja na kupata pesa ya kuendelea kutumia application mbalimbali pamoja na kupata pesa ya nauli kuhudhuria interview ninapokuwa nimeitwa.

Nimekaa na kutafakari nimeona nianzishe kibanda cha uwakala wa Tigo pesa, Mpesa na Airtel money.Nimejaribu kufuatilia nimeambiwa tigo pesa kwa sasa hawachukui mawakala wapya, ila wiki iliyopita nilifika ofisini kwao wakaniambia ninaweza kupata nafasi maana wanamchakato wa kuwapa watu namba kutoka kwa mawakala wanaoonyesha kutokuzitumia ila inabidi uwe na Tin number pamoja na lessen ya biashara na kianzio cha milioni moja. MPESA pia wakasema kianzio ni laki tano, AIRTEL MONEY ni laki mbili na nusu ila requrement zingine zinafanana. Naomba mnisaidie mambo yafuatayo.

(1) Ni jinsi gani ninaweza kupata mkopo wa kukamilisha requrement hizo? na wapi naweza kupata mkopo

huo(SIMILIKI MALI YOYOTE HISIYOHAMISHIKA)

(2) Kwa wenye uzoefu na kazi hii inawezachukua muda ganikulipa mkopo husika matharani kama nikikopa milioni

mbili ilikuanzisha mradi huu?

(3) Nina TIN NUMBER niliyoipata kipindi naomba lessen ya udereva je hii inafaa kwenye ile requrement ya kuwa

na tin number au siyo ya namna hii? Pia mchakato wa kupata lessen ya biashara TRA ukoje?inaweza nigharimu

shilingi ngapi na inaweza chukua muda gani kuipata?

(4) Nimeambiwa unaweza nunua line ya tigopesa kwa muda aliyenayo lakini yeye pengine kwa sasa haitumii na

katika kupeleleza naambiwa zinauzwa kati ya laki nne na laki saba je ukisha nunua kwa mtu hivi unaenda

tena ofisi za tigo ilikuweka kile kianzio cha milion moja au ndo basi kwa kuwa muhusika aliweka kipindi

anaichukua?

Natanguliza shukurani wadau michango yenu ni muhimu sana kwangu.
 
call number 0653660669/0733 660669

Kwa msaada zaidi!
karibu
Ndugu una wazo zuri la kijiajiri lkn mkopo hutweza kupata mpaka uwe na dhamana au biashara tayar! Pili hii kaz ya uwakala mim nina uzoefu nayo kma miaka 3. Sema sas hv mawakala wamekuwa weng sna so hailip tna kma mwanzon na pia kod zmekuwa nyng sna! So inatakuwa uwe na mtaji mkubwa kama mil 5 au zaid ili mteja asije akakosa hela na pia kutoa pesa kubwa ndo unapata kamishen kubwa.
Tatu unawe kununua line kwa mtu na hakuna haja ya kwenda tna tgo au vda kuweka pesa.
Nne tin namba ya lesen ya udreva haiwez kutumika kwnye biashara so lazima uaply tin nyngne pamoja na lesen ya biashara!lesen ni kama sh. Lak moja hv au zaid! Pia lazima biashara yko uilocate sehemu yenye wateja weng vingnevyo unaweza ukute kwa mwez mzima unapata kamishen elfu 70 au lak1. Ahsante sna!
 
Habari wakuu, Mimi ni graduate ninaeendelea kusaka ajira. Katika kipindi hiki cha utafutaji wa ajira nimekuwa sina kazi yoyote ya kuniingizia kipato chochote cha kupata pesa kidogo kwa ajili ya matumizi yangu ikiwa ni pamoja na kupata pesa ya kuendelea kutumia application mbalimbali pamoja na kupata pesa ya nauli kuhudhuria interview ninapokuwa nimeitwa.

Nimekaa na kutafakari nimeona nianzishe kibanda cha uwakala wa Tigo pesa, Mpesa na Airtel money.Nimejaribu kufuatilia nimeambiwa tigo pesa kwa sasa hawachukui mawakala wapya, ila wiki iliyopita nilifika ofisini kwao wakaniambia ninaweza kupata nafasi maana wanamchakato wa kuwapa watu namba kutoka kwa mawakala wanaoonyesha kutokuzitumia ila inabidi uwe na Tin number pamoja na lessen ya biashara na kianzio cha milioni moja. MPESA pia wakasema kianzio ni laki tano, AIRTEL MONEY ni laki mbili na nusu ila requrement zingine zinafanana. Naomba mnisaidie mambo yafuatayo.

(1) Ni jinsi gani ninaweza kupata mkopo wa kukamilisha requrement hizo? na wapi naweza kupata mkopo

huo(SIMILIKI MALI YOYOTE HISIYOHAMISHIKA)

(2) Kwa wenye uzoefu na kazi hii inawezachukua muda ganikulipa mkopo husika matharani kama nikikopa milioni

mbili ilikuanzisha mradi huu?

(3) Nina TIN NUMBER niliyoipata kipindi naomba lessen ya udereva je hii inafaa kwenye ile requrement ya kuwa

na tin number au siyo ya namna hii? Pia mchakato wa kupata lessen ya biashara TRA ukoje?inaweza nigharimu

shilingi ngapi na inaweza chukua muda gani kuipata?

(4) Nimeambiwa unaweza nunua line ya tigopesa kwa muda aliyenayo lakini yeye pengine kwa sasa haitumii na

katika kupeleleza naambiwa zinauzwa kati ya laki nne na laki saba je ukisha nunua kwa mtu hivi unaenda

tena ofisi za tigo ilikuweka kile kianzio cha milion moja au ndo basi kwa kuwa muhusika aliweka kipindi

anaichukua?

Natanguliza shukurani wadau michango yenu ni muhimu sana kwangu.

Wazo lako ni zuri lakini kuna vitu fulani umesahau:
  1. kodi ya pango kwa busines pemises
  2. hiyo laki saba unayompa mwenye laini ya TIGO pesa niza kuinunua tu ankupa ikwa haina float /salio ndani yake hivyo inabidi uweke float sasa ili uweze kuhudumia wateja kuweka na kutoa pesa.
  3. hiyo TIN yako yaa udereva nenda nayo ofisi ya TRA iliyo karibu nawe uwaambie unataka kuanzisha biashara ya M-pesa wataibadili kuwa ya biashara.
  4. masharti ya UWAKALA wa TIGO pesa ni kwamba it must not be stand alone business kwa sababu haitakulipa kwa sababu commission ni ndogo sana na mbaya zaidi sasa hivi serikali imeingiza huko kodi ya 2% ya zuio inayokatwa juu kwa juu.
  5. sasa kwa sababu utaweka na bidhaa nyingine kwenye frame yako kama line ,cvers charger kwa kadiri mtaji utavyokuwa unaongezeka TRA Watakudai kodi ya shs 100,000/= kama mapato yako kwa mwaka mzima yatafikia 4,000,000/= vinginevyo wanatakiwa wasikudai chochote. sasa hapo kwenye kuthitisha TRA kuwa mapato yako kwa mwaka hayafikii 4m utaomba yesu arudi kuwahukumu wazima na wafu kwa adha utakayokutana nayo. PEROD!
 
Asante sana Matshs kwa kujitoa kwako, Nitakupigia ili uweze kunisaidia Mkuu
 
Wakuu nashukuru sana kwa ushauri wenu, kwa hakika umesheheni kila aina ya information nilizotakiwa kuwanazo kabla ya kuanzisha mradi huu. Kutokana na jinsi nilivyofuatilia taarifa za kuanzisha mradi huu na ushauri wa kiuzoefu nilioupata kwenu naona kama mradi huu unakuwa na ugumu wake. Naendelea kusugua kichwa kuona namna ya kufanya ila nitafurahi zaidi kuendelea kupata ushauri zaidi kutoka kwenu wakuu! Endeleeni kunipa msaada mdogo wenu.
 
Back
Top Bottom