Mkuu inategemeana, na wewe kama director ni vizuri ukajilipa mshahara na kama basi sio mshahara basi benefit zingine kama Perdiem na kazalika na hii huwa ni kabla ya faida, yaani faida ni baada ya kutoa kila kitu ikiwemo mshahara wako.
Na biashara ikiwa kubwa unaweza set kabisa mshahara wako na sio unajipangia, no unatafuta watalaamu wa HR wanakupangia, na mshahara utakuwezesha wewe kujikimu mfano kulipa ada za shule, na matumizi milengine, Ila ukiwa Kama mkurugenzi utakuwa na mshahara pamoja na gawio la faida.