nacte walinipangia chuo cha Tanzania training center for international courses ya clinical medicine. lakini kumbe iko chuo hawatoi clinical medicine ila wanatoa AMO assistant medical officer. leo nimeenda makao makuu ya nacte wakaniambia ni kweli baraza na wizara ya afya ndio walifanya makosa kukiweka iko chuo.. lakini wakaniambia nifanye tena application kwa third round na vyuo vinavyotoa clinical medicine vimebaki vitatu tu na kuna applicants wengi sana wanaoomba nafasi na kibaya zaidi jumla ya nafasi ya hivyo vyuo ni 12 na wombaji ni 389.
je hii ni haki kweli nilivyofanyiwa? niliomba wanifanyie transfer wamekataa. naombeni ushauri please