Msaada: Wachawi hua wanafanyia nini nguo wanazochukua?

Hamis Juma

JF-Expert Member
Nov 4, 2011
2,229
2,272
Habarini wakuu,

Ni muda sasa nguo zao zimekua zikipotea katika mazingira ya kutatanisha ama kuchanwa na vipande kutokuonekana. Kipindi cha mwanzo nilihisi panya, lakini ninejiridhisha haiko hivyo. Ni hawa wataalamu jadi "wachawi" wakichukua.

Siku za hivi karibuni nimekua nikikuta hata viatu nimekeishawekewa soksi, kali zaidi jana wameniwekea vishikizo katika shati (nilinunua shati jipya ili nivae, nikalinyosha, asubuhi nakuta vishikizo/vifungo viwili hakuna na kimoja kimewekwa ambacho si cha kufanana na ile shati)

Cc: mshana jr, hr666
 
Wengi watakuja kukupinga na wenginekukubeza kama sio kukupuuza kabisa lakini ukweli unabaki pale pale tu kwamba "aisimuliaye mvua imemnyeshea" na "huwezi kwenda msalani bila kubanwa na haja"...pole sana mkuu nakushauri uende ukaperuzi kwa Sangoma tu ili ujue nani muhusika.
 
kuna teja kabeba lol

nakutania mkuu,ngoja mshana na mzizi mkavu waje....
 
Nyumba ninaishi peke yangu, nikilala nafunga milango. Ndani hakuna uzi wala sindano, ningesema nilishona usingizini... Nani mwingine atafanya hivo zaidi ya mchawi
 
Wengi watakuja kukupinga na wenginekukubeza kama sio kukupuuza kabisa lakini ukweli unabaki pale pale tu kwamba "aisimuliaye mvua imemnyeshea" na "huwezi kwenda msalani bila kubanwa na haja"...pole sana mkuu nakushauri uende ukaperuzi kwa Sangoma tu ili ujue nani muhusika.
Kwenda kwa Sangoma ishu nyingine, maana sasa hivi wamejaa kwelikweli, halisi hajulikani wala asie halisi hajulikani
 
Kuna jirani anakufanyishia physically ili uone tu ni uchawi
Naishi peke yangu, hii nyumba kama sijafungua mlango huwezi ingia maana funguo zote ninazo mimi... Nikilala hua nafunga milango vizuri, sasa huyo jirani usiku anapita wapi
 
Back
Top Bottom