Wekeza kwenye kilimo cha kisasa lima hasa maharage, ndizi za biashara mbivu, parachichi pia unaweza kufanya kilimo cha miti wakati unaandaa na kusubiri kwa miaka 6-8 ili uvune anzisha kampuni ya kuuza mbao na kutengeneza furniture za kisasa ambazo zina chapa yako ya hapa ndani na nchi jirani. pia unaweza kuanzisha kiwanda cha mbolea.
Tanzania Kilimo kinalipa pia tuna upungufu wa mbolea kwa 60% kwasababu nyingi tunaimport kutoka nje hapa kwenye kiwanda ukifanikiwa utaweza kuziudumia hata nchi za rwanda, burundi, uganda na congo ila all in all kama hauna njaa wekeza kwenye kilimo cha muda mrefu kama miti, ndizi na parachichi.
Pia unaweza kuwekeza kwenye kiwanda cha unga maana wabongo tunazaliana na kula lazima tule ufunge vizuri uwe na chapa inayovutia watu wengi wamewekeza kwenye sembe wewe unaweza wekeza kwenye dona, muhogo, mtama pia ulezi focus ni kuwa na kitengo kizuri cha masoko utatoboa.
Mimi nipo kwenye kilimo cha miti ndizi, maharage, parachichi na ufugaji wa sato(bwawa) sijawahi kujuta.