Allydasmartboy001
JF-Expert Member
- Jul 14, 2018
- 604
- 218
Kwanza kabisa kabla sijaendelea na penda kusema asante kwa wale wote walio ni sahau mimi ni yule mwanafunzi niliyepata 1 ya 7 na nikakosa chuo hadi hawamu ya 3 ndipo nikaja hapa kuomba ushauli na nina shukuru mungu nika apply chuo cha KCMC na mungu akanisaidia asante sana ndugu zangu na bila kumsahau dada yangu EVLINA kwa ushauli. Leo nimekuja na tatizo lingine la rafiki yangu ingawa niliwahi kuweka machapisho kadha lakini siku pata maoni mazuri sana ingawa nina washukuru ila nina rudi tena. Rafiki yangu tulisoma wote PCB ingawa yeye matokeo yake haya kuwa mazuri sana na alikosa awamu zote 4 alipata 2 ya 12 na matokeo yake yalikuwa CHEM C BIOLOGY C NA PHYSICS S. Baada ya kukosa hawamu zote 4 mpaka leo yupo bado nyumba kwa kusubilia hawamu nyingine ila hapa kati kati tulipata wazo la kujalibu kuangalia Uganda. Yeye shida yake kusoma course ya medical doctor au phamacy hasa hasa katika chuo cha makerere. Tatizo tulikuanalo mpaka kuja hapa kuomba msaada. Tulitaka kuuliza je kwa hayo matokeo anaweza pata chuo uganda na kwenda kusoma hizo course???. Tunazo namba za chuo cha makerere na email zao lakini tukipiga namba zao hawapokei na hata email hawajibu tumeangaika sana lakini tunakosa haya majibu. Sisi shida yetu kujua tu kwa anajua system ya elimu ya uganda au hata kwa anayesoma katika vyuo vya uganda kama yeye mwenyewe au ndugu yake naomba atusaidie kwa hili. Sisia shida yetu ni mmoja tu kujua kama anasifa za kusoma katika vyuo vya uganda na hizo course anazo zitaka. Asanteni sana ndugu zangu na nina imani mtatusaidi sisi wadogo zenu
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app