Msaada wa ushauri

Msaada wa ushauri

kedekede

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
5,335
Reaction score
7,745
Wataalam nawasalimu,
Moja Kwa Moja nakuja kwenye tatizo.
Juzi alhamis mwanangu mdogo alirudi kutoka shule akiwa anachechemea kidole gumba hakigusi chini anakipandisha juu ya nyayo.
Nilimuangalia nikaona kama ana mwiba umemchoma.Sikumtoa nikawaza nimuwekee utomvu wa papai Ili iwe rahisi kuutoa asubui.
Bahati mbaya nikakosa utomvu wa papai.
Asubui kukawa na kama Usaa umetunga.Aligoma kutumbuliwa nikampeleka shule.Kwa vile watoto wanaamini walimu nikawaambia wamtumbue akatumbuliwa na toothpick zile ambazo mpaka utoe kipakti.
Akashinda fresh ila usiku akawa analialia mwisho akalala.
Leo akaamka na kama lengelenge ila mida tangu saa Moja asubui Hadi sasa linekuwa kubwa na kama ameungua.Kuna mama mmoja ameshtua kidogo kuwa inawezekana nyoka aliulamba huo mwiba ndio maana imetokea Hali hiyo na tusimtumbue.
Yule mama simuamini but what is this?Sishindwi kumpeleka hospitali ila anaenda kupimwa Nini maana sasa hivi Kila mtu ni mtaalam.
Natanguliza shukurani Kwa ushaur.
 
Attachments

  • IMG_20230211_143824_893.jpg
    IMG_20230211_143824_893.jpg
    529.5 KB · Views: 8
  • IMG_20230211_143824_893.jpg
    IMG_20230211_143824_893.jpg
    529.5 KB · Views: 8
Unamjua nyoka au unamsikia ingekua ni sumu ya nyoka lazima mwili mzima uwe na homa Kali huenda kipande hakijaisha kama ni nyoka mguu unaweza kuoza mpeleke kwa doctor haraka sana
 
Muwaishe hospital vitu vingine sio vya kuuliza mitandaoni...
 
Yaani kidole cha mtoto kimevimba na bado unampeleka shule ili walimu wakusaidie..mkuu hauko serious embu mpeleke mtoto hospital akapate matibabu kabla mambo hayajamzidia mtoto acha kucheza na afya ya mtoto ...kumbuka afya ni mtaji namba moja
 
Anaenda kupimwa nn mkuu?@kunguru wa unguja na Gilly
 
Wataalam nawasalimu,
Moja Kwa Moja nakuja kwenye tatizo.
Juzi alhamis mwanangu mdogo alirudi kutoka shule akiwa anachechemea kidole gumba hakigusi chini anakipandisha juu ya nyayo.
Nilimuangalia nikaona kama ana mwiba umemchoma.Sikumtoa nikawaza nimuwekee utomvu wa papai Ili iwe rahisi kuutoa asubui.
Bahati mbaya nikakosa utomvu wa papai.
Asubui kukawa na kama Usaa umetunga.Aligoma kutumbuliwa nikampeleka shule.Kwa vile watoto wanaamini walimu nikawaambia wamtumbue akatumbuliwa na toothpick zile ambazo mpaka utoe kipakti.
Akashinda fresh ila usiku akawa analialia mwisho akalala.
Leo akaamka na kama lengelenge ila mida tangu saa Moja asubui Hadi sasa linekuwa kubwa na kama ameungua.Kuna mama mmoja ameshtua kidogo kuwa inawezekana nyoka aliulamba huo mwiba ndio maana imetokea Hali hiyo na tusimtumbue.
Yule mama simuamini but what is this?Sishindwi kumpeleka hospitali ila anaenda kupimwa Nini maana sasa hivi Kila mtu ni mtaalam.
Natanguliza shukurani Kwa ushaur.
Habari!

1: Kuvimba ni athari ya kuumia kwa sehemu husika. Ingawa kwa kuwa kuna nafasi ya ngozi kuwa wazi, bakteria wanaweza kupata nafasi ya kuanzisha maambukizi.

2: Kuna haja ya kufahamu aaili ya kitu kilichomuumiza mtoto na eneo pia. Hii husaidia kwenye aina na kiasi cha matibabu.

3: Mtoa huduma ya afua anaweza kuongea jwa urafiki na mtoto hivyo kueleza mazinhira ya tatizo.

NB: MUHIMU KUMFIKISHA MTOTO KITUO CHA AFYA.
 
Back
Top Bottom