Msaada wa ushauri, jinsi ya kupunguza hasira

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Salaam wanaJF,

Katika mishemishe zangu mtaani Leo nimekutana na rafiki yangu wa kitambo sana na katika kujuliana hali akaniomba msaada ni kwa jinsi gani anaweza kupunguza hasira maana amekosana na kila mtu mtaani kwao.

Ni rafiki niliyekutana naye mkoani Mara, kwa mara ya kwanza na ndiyo kwao ila kaja maeneo yetu kusaka maisha, Jamaa alikuwa na mke ila kafukuza baada ya kuzozana kwa muda na kumpatia kipigo mke kamkimbia pia mtu yeyote akimkosea ata kama ni kosa dogo huwa anatoa kipigo.

Hivi sasa kakimbilia huku Jijini kujipanga upya.

...Nakaribisha ushauri na maoni...
 

DAFU NA NDIMU

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,456
2,000
Mi sijui nifanyaje niongeze hasira?
Mtu ananitukana halafu mi nampotezea tu.
Sana sana nitacheka na kuondoka, ingawa naweza kuja kukasirika siku inayofuata kwa sekunde tu, then nasamehe.
Akinipora kitu changu mi naishia kumshukuru Mungu
Jamani, nifanyaje ili niongeze hasira?
 

chavdy

Senior Member
Feb 29, 2016
181
250
Mshauri wakati akiwa na hasira afanye mazoezi huku akiwa anasikilia mziki husaidia sana kupunguza hasira
Njia nyingine ni kukaa sehem tulivu kikiwa hakuna mtu kama uwanjani hivi na kuongea mwenyewe kwa nguvu( sijawahi kujaribu ila hiyo ni kutoka kwa wataaluma wanasema husaidia kupunguza stress na harisa pia ) yangu hayo tu.
 

Jaby'z

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
3,813
2,000
mwambie akipata hasira asiwe anaendelea kukaa karibu na mazingira yaliyomsababisha akapata hasira..
 

Jamalm335

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
2,258
2,000
muambie afanye sana ibada kwa imani yake. Hasira hutokana na shetani na palipo na ibada daima pana Mungu na shetani hakai hapo kamwe.
 

Emojis

Senior Member
Jan 4, 2017
192
250
Njia nzuri ya kuzuia hasira ni kunywa maji mdomon asiyameze mpaka hasira yake itakapoisha akizoea mara kwa mara utajikuta anaweza kbixa kucontrol hasira yake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom