Msaada wa tiba wa tatizo hili?

Mwanakanenge

Member
Nov 25, 2012
75
16
Habari za leo wana jamvi,
Naomba kuleta kwenu suala hili kwa lengo la kupata ushauri juu ya tiba,nina mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 2 na miezi 7,tatizo linalomkabili ni kutoshuka kwa korodani zake zote mbili,mara ya kwanza korodani moja ilikuwa inaonekana ukiishika unaisikia baada ya kufanyiwa operesheni ili kushusha ya pili,hali imekuwa tofauti zote mbili hazionekani tena,hospitali wanasema afaniwe tena operesheni ya pili,Je kwa yoyote mwenye ueleewa na tatizo kama hili na njia za kulitatua.
 
Wengi wetu hua hatuamini dawa za kienyeji kama zinatibu. Lakini kuna baadhi ya magonjwa hutibiwa kirahisi sana na dawa za kienyeji.
Tatizo la mwanao ukiwafuata wabibi wazoefu watakusaidia kirahiiiisi hata bila ya hiyo op. Kwa maradhi hayo ni mchango. Na ikichukua mda mrefu mtoto atakuwa anapatwa na maumivu makali na kulia sana.
Tatizo hili huwa lipo na kwa watu wazima pia kwa jina lingine huitwa mshipa wa ngiri. Kwa hospital tiba yao ni kwa njia ya upasuaji.
 
Back
Top Bottom