Msaada wa technician: Laptop Dell XPS L502 X

Msaada wa technician: Laptop Dell XPS L502 X

Zainab Tamim

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Posts
1,293
Reaction score
583
Laptop yangu Dell XPS L502 X, Core i7

Inaniletea message kuwa Hard Disk (Toshiba) ina matatizo. Na imekuwa slow sana wakati wa kuiwasha na kuitumia. Ninatafuta technician ataerekebisha haya:

- Hiyo hard disk

- Speaker zake sijui zimechanika kwa ndani hazitoi sauti kama zamani na zinakoroma, ina JBL speakers built in. Zirekebishwe.

- Battery nilibadilisha lakini hii niliyobadili haijakaa muda (ni replacement part siyo original) haijakaa hata miezi mitatu haiweki charge kama zamani, zamani nilikuwa ninaitumia laptop hata masaa matatu bila ku recharge, sasa hivi hata dakika 15 haikai. Nitahitaji battery bora.

- Niliwekewa MS office ambayo inaniletea message kuwa inataka iwe activated, kurekebisha hii na kuweka latest version ya MS Office.

Technician ambae atakuja na kuirekebisha hayo itakuwa ni hapa hapa ofisini kwangu Sinza na sikubali iondoke nje ya hapa ofisini kwani nimeshalizwa laptop moja na fundi.

Technician aje kikamilifu kama itahitaji backup na chochote katika hayo niliyowaeleza, nenda rudi si vyema na kuwachwa bila laptop pia si vyema.

Ninaomba estimation ya hayo marekebisho nijipange.

Aliye tayari awasiliane na Mzee Abdul 0756803528 kwani mimi sijui sana mambo haya.
 
Mkuu upo Sinza eneo gani nije kufix kila kitu hapoo?

mkuu nahisi haupo serious kikazi sababu mzee kashaweka namba yake ya simu cha msingi wewe chukua namba mpigie ukafanye kazi ukibakia kupost tu hapa jamvini wenzio watachukua namba wanampigia wanaenda kupiga kazi bila hata kuandika kitu hapa jamvini
 
Kwa wale wote waliowasiliana nami napenda kuwajulisha kuwa nimepata technician kupitia tangazo hili hili na tumekubaliana ataishughulikia laptop yangu Jumatatu.

Asanteni sana na asante JF.
 
Wadau,

Kuna kijana alikuja kunitengenezea laptop yangu baada ya kuona hili tangazo, bahati mbaya nimepoteza mawasiiliano nae naomba awasiliane nasi kwa 0625249605.
 
Back
Top Bottom