Msaada wa shule ya sekondari

Msaada wa shule ya sekondari

MKABESA

Member
Joined
Oct 15, 2011
Posts
6
Reaction score
2
Wanajamvi, habari zenu. Mimi ni mzazi wa mtoto mwenye tatizo kitaalamu wanaliita cerebral palsy. mwanangu amemaliza darasa la saba katika shule ya kiingereza (English Medium). Katika mtihani wake wa darasa la saba Wizara ya Elimu ilimsaidia kwa kumuongezea kumpa muda wa ziada, pamoja na kumpa fursa ya kujaza ABC badala ya ku-shade kama walivyokuwa wanafanya wenzake. mwanangu anasikia na anaelewa vizuri hata kujieleza yeye mwenyewe anaweza japokuwa matamshi yake hayanyoki sawasawa. Tatizo lake kubwa ni katika kuandika, kwani anatetemeka mkono.

Naomba msaada ili kuweza kumtoa mwanangu katika hatua hii na kuendelea na masomo ya sekondari.yeye mwenyewe anapenda kusoma ila mpaka sasa shule tulizokwenda kuomba nafasi hawajampokea. NAOMBA SANA MSAADA WENU. ASANTE
 
Back
Top Bottom