Sidhani Javascript ni program unayoinstall kama standalone program bali itakuwepo kwenye computer yako kama web browser (Internet Explorer, Firefox) ipo installed.
Labda kama swali lilikuwa ni software ipi nitatumia kuandika javascript pengine wadau wangekupa hizo programs.
Tupe maelezo yakinifu unaitaka hiyo javascript program ili uifanyie nini? Kwa kukusaidia tuu ni kwamba Javascript siyo program bali ni client site language (japokuwa siku hizi kuna sever side JS) yaani inakuwa executed kwenye browser ili kuleta a dynamic user friendly experience. Sasa tueleze vizuri unachotaka maana inawezekana unaongelea Javascript engine tukidhani hujui unachoongea, unaposema program, wakati wewe ni pro.