Msaada wa neno AIRPORT kwa kiswahili tafadhali

Nanoli

JF-Expert Member
Oct 15, 2015
3,735
5,970
Hi,

Wakuu naomba mnielimishe maana ya AIRPORT kwa kiswahili tafadhali... Naipenda lugha yangu ya kiswahili, hivyo napenda ninapozungumza lugha hii nisichanganye na lugha ya kigeni (kiswanglish)... Kwa yeyote anayejua naomba msaada wa neno hili

Nawasilisha....
 
duh ni kweli ulikuwa hujui au makusudi??? hata mtoto wa chekechea anajua maana ya airport
 
Hujanijibu mkuu, AIRPORT kwa kiswahili inaitwaje? Najua utasema UWANJA wa ndege, naomba jina linalojitegemea kama AIRPORT....
 
Hi,

Wakuu naomba mnielimishe maana ya AIRPORT kwa kiswahili tafadhali... Naipenda lugha yangu ya kiswahili, hivyo napenda ninapozungumza lugha hii nisichanganye na lugha ya kigeni (kiswanglish)... Kwa yeyote anayejua naomba msaada wa neno hili

Nawasilisha....
Upara/kipara
 
Mbona wameshakujibu inaitwa Uwanja wa ndege au unapenda ubishi? Au unataka utafsiri neno moja moja la AIR na PORT?
Lengo langu sio ubishi mkuu, ukiangalia wenzetu jina lao halijawekwa moja moja AIR... PORT, nafikiri jina kama jina haliwi na mtengano wa maneno, bali husimama jina kama jina,... Mfano hivi karibuni BAKITA wameweza kutuletea neno MUBASHARA (LIVE) hapo awali hatukuwa na neno la kiswahili... Tulikua tukisema hivyo hivyo kwa maana ya MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA,... Sawa ungeulizwa neno LIVE kwa kiswahili linaitwaje, huwezi sema MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA, bali utasema MUBASHARA...... nami nataka kujua neno AIRPORT kwa kiswahili linaitwaje?
 
Namuunga mkono mtoa mada, Neno Uwanja wa ndege laweza kuwa na maana zaidi ya moja.
1. si kila uwanja wa ndege au sehemu inayoitwa kiwanja cha ndege ndege ulaya hutua na kuruka na kutua
2. Kama ni uwanja wa ndege, je ni ndege gani? Kunguru, mwewe, tai, kuku, njiwa au bundi?
3. Airport ina miundo mbinu yake kuwezesha ndege ulaya kutua na kuruka salama. Uwanja tu hautoshelezi mambo hayo.
Tusiishi kwa mazoea, pia ni vizuri tukuze lugha yetu.
 
Nashukuru mkuu kwa ufafanuzi wako nzuri, umenielewa mno.... Tumekosa neno hapa, hatuna jina Lake la kiswahili... Kama yupo anayejua atujuze tukuze lugha yetu.
 
Hi,

Wakuu naomba mnielimishe maana ya AIRPORT kwa kiswahili tafadhali... Naipenda lugha yangu ya kiswahili, hivyo napenda ninapozungumza lugha hii nisichanganye na lugha ya kigeni (kiswanglish)... Kwa yeyote anayejua naomba msaada wa neno hili

Nawasilisha....
"anga tua" (kiswahili) - Airport. (english)
 
Hujanijibu mkuu, AIRPORT kwa kiswahili inaitwaje? Najua utasema UWANJA wa ndege, naomba jina linalojitegemea kama AIRPORT....
Si wakati wote lugha au maneno yanakidhi mantiki. Hata hilo neno lako la kiingereza "airport" halina mantiki sana hata kwenye kiingereza chenyewe! Air inaweza kuwa na maana ya hewa au anga. Sasa ukitizama sana air-port haina mantiki kwa sababu sote tunajua huo uwanja au sehemu inayoitwa airtport haipo angani na wala sio kwa ajili ya hewa bali ni kipande au eneo la ardhi (aghalabu) kwa ajili ya ndege kutua kutoka angani na kupaa kwenda angani.

Lugha kwa sehemu kubwa ni sauti za nasibu (zinazuka tu!).
 
Nashukuru mkuu kwa ufafanuzi wako nzuri, umenielewa mno.... Tumekosa neno hapa, hatuna jina Lake la kiswahili... Kama yupo anayejua atujuze tukuze lugha yetu.
Umenena vyema kiongozi. Tukubali tu kwamba hatuna kiswahili cha neno AIRPORT, kama ambavyo hatukuwa na kishwahili cha neno LIVE.
Pia wadau wafahamu kwamba siku zote lugha inakua, na inakwenda na wakati.
 
Back
Top Bottom