Habari wakuu
Katika maisha kuna mambo mengi sana ambayo binadamu ameumbiwa ili kumsaidia lakini yampasa kuwa na maarifa fulani fulani ili kuweza kugundua kwa wakati.
Nirukie moja kwa moja kwenye mada, nimekuwa nikiota ndoto zinazohusu.matukio niliyofanya zaidi kipindi cha nyuma nikiwa mdogo miaka ya 1998~2007 hili jambo linajirudia rudia takribani miaka 3 sasa sioti ndoto mpya bali ubongo wangu unaniletea matukio ya zamani tu.
Hii hali imeanza kunipa wasiwasi najiuliza kulikoni kwa nini nafanya mambo mengi na watu wapya lakini nikilala sioti mambo ya hivi karibuni ama siku husika naishia kupata ndoto za miaka 10+ nyuma. changa moto ni kuwa hakuna ndoto. maalum ambayo inajirudia zaidi yaani ni mchanganyiko leo unaota tukio fulani upo primary unacheza na wenzako siku ingine unaota tukio la miaka kadhaa mbele ama nyuma zaidi
Kuna kitu kiliwahi kunitesa sana nakumbuka mwaka 2016/17 nilikua naishi wilaya ya Lushoto pale mjini mkoa wa Tanga kuna kipindi watu walikua wananifananisha na polisi ambaye anewahi kufanya kazi apo yaani ukipita unaitwa fulani vipi za siku mingi uko wapi siku hizi?
Haikuishia apo watu wengi sana wakawa wananiita na kusema wamenifananisha na ndugu yao zaidi ilikua ni watu wa makamo wakubwa kwa wazee lakini nikawa nawakatalia nawaambia sio mimi lakini ilifika mahali ikawa kero kila mtu ananifananisha.
kuna kipindi nikawaza nibadilishe lifestyle ama namna ya mavazi lakini bado watu kila mara wananifananisha na ndugu zao juzi kati nimefika mwanza naingia bar kupata chochote mara akanipokea jamaa mmoja kwa. mbwebwe na kunichangamkia kama vile tunafahamiana nikahisi labda ni tapeli anataka labda nimpe ofa ya bia lakini haikua ivo jamaa akaniuliza wewe si ndugu yake na fulani.....tumetoka kumzika mdogo wake juzi eneo fulani...kiukweli hayo maeneo sikuwa nayafahamu nikamjibu hapana akaniacha na akaendelea kula bia zake alikua anajiweza kwa maongezi aliokua anafanya na wenzake atakua ni mwalimu.
Siku ingine nikaenda tena mahali palepale nikakutana na mtu mwingine gafla ananiuliza gari yako imetoka apa nani anaiendesha ? leo utanipa lifti? kiukweli kulikuwa kuna gari kama mbili zilitoka mahala pale muda ule mimi naingia nilishangaa kisha nikamjibu itarudi basi jamaa akaanza kuongea na mimi kama vile tuna faamiana.
akaniuliza leo unaanza kununua wew au nianze mimi nikamwambia aanze yeye huku nikijiuliza maswali kibao kichwani mwangu basi akamwambia waiter anipe bia moja baada ya mimi kumaliza ambayo nilikua nimeagiza mwanzo then akaagiza ya 2 na ya tatu mwisho nikamnunulia bia 2 jamaa alionekana ameanza pombe mapema ilikua ni siku ya juma pili kwani alikua anagawa offer sana kwa bar maids kama lofa fulani......
mwenye uelewa wa haya mambo please tueleweshane kwani unaweza kujihisi unaishi nyuma ya wakati natamani ningekuwa angalau naota mambo yajayo lakini kuota yaliopita yanakua yanasababisha mtu kukumbuka ulikotoka na huweza kusababisha kulipa visasi wakati mwingine kukufanya uwe na huruma sana. kiufupi unakuwa unashindwa kuwa unavotaka ama kupaswa kuwa.