Msaada wa namna ya kubadili jina la kwenye cheti cha kuzaliwa

Smith Rowe

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
3,316
5,442
Salaam

Naombeni msaada nataka kubadili jina lililoko kwenye cheti cha kuzaliwa lifanane na nililotumia kwenye kusoma.

Mwenye kujua utaratibu naomba anieleze.
 
Mwenye kuelewa naomba anisaidie
Ingia RITA kwenye website yao kuna fomu utadownload na kuijaza na kuwapelekea. Pia mule mule kuna gharama ya kulipia imeonyeshwa, nafikiri ni shilingi 3000 sipo sure zaidi.

Fanya hivyo.
 
Nenda mahakaman Kuapa.utapewa maelekezo vizur na utaenda RITA kwa ajili ya kupata cheti ukitakacho kwa majina hayo mapya.itakukost kulipia gharama huko RITA .sio kubwa ila inawezekana
 
Nenda kwa mwanasheria utajaza jima unalotaka kutumia hiyo fomu inaitwa deed poll mwanasheria atakujazia atagonga muhuri utaendawizara ya ardhi utakugongea muhuri wataiweka kwenye system utatumia jina ulilochagua bila tatizo
 
Nenda kwa mwanasheria utajaza jima unalotaka kutumia hiyo fomu inaitwa deed poll mwanasheria atakujazia atagonga muhuri utaendawizara ya ardhi utakugongea muhuri wataiweka kwenye system utatumia jina ulilochagua bila tatizo
Naongezea: kwa huyo msajili wa nyaraka utalipia shilingi elfu 32.Pamoja na passport size kwa kila nakala ya deed poll
 
Nilikua na tatizo kama lako lakini nililimaliza hivi:
Nilienda kwa msajili wa vizazi na vifo katika wilaya niliyo zaliwa na nikamweleza tatizo langu alinipa form nikajaza, nikaandika barua ya kuomba kubadilishiwa jina lisomeke kama kwenye vyeti vya shule na nikaambatanisha na copy ya vyeti.
Nikapewa control number nikalipia 6500 na baada ya hapo nikapeleka risiti nikasubiri kwa wiki 2 nikaenda chukua cheti kiko kama nilivotaka kiwe.
 
Back
Top Bottom