Ningelikuwa ni mimi, ningelieanza kwa utafiti mdogo wa hizo biashara mbili na kuangalia vifuatavyo:
i- Ipi kati ya hizo biashara mbili watu wanaihitaji zaidi?
ii- Ukubwa wa hitaji hilo ikoje?
iii-Je mtaji ninao wa kuanzisha hitaji likiongezeka nitauongezaje ili nisipoteze soko
iv- inaweza ikawa inahitajika je malighafi yake inapatikana kwa urahisi?
v- je ninaweza kupata sehemu ya kuiweka ambayo wateja wataiona vizuri ili iwe rahisi kwangu kujitangaza
vi- ushindani ukoje na nina jiandaa vipi katika kuhakikisha nitadumu kwenye ushindani, nitajitofautishaje na wenzangu ili wateja waweze kuja kununua katika biashara yangu
Kila la heri Sharura!