Wakuu habari za majukumu ya kulijenga taifa letu.
Hivi karibuni nilipata kuhama sehemu niliyokuwa na kuhamia sehemu nyingine kikazi, na Mungu ni mwema nafasi (cheo) kilikuwa ni cha juu tofauti na awali na chenye masirahi zaidi.
Sasa nmelipoti huku na kwakweli niliwajulisha ndugu zangu wa karibu na walinipongeza, mke wangu pia alimjulisha mama yake (ndo mtu yuko nae karibu zaidi na hawafichani kitu)
Sasa nikapanga safari kwenda nyumbani hivi karibuni na nilimweleza mke wangu kuwa nitaenda hom kuwasalimia.
Leo katika maongezi wife amenieleza kuwa juzi aliota ndoto kuhusu mimi na haikuwa nzuri, na katika ndoto kuna mtu alimueleza vitu hivyo ananiomba nikifika niwe makini sana, nimshirikishe Mungu na nisile kitu bila kuomba.
Nikajalibu kumdadisi ili anisimulie lakini sikufanikiwa, alikataa kabsa na kusema hawezi kunisimulia.
Wazo likanijia na kuhisi hii ndoto ni lazima amemsimulia mama yake kwani ndiyo mshauri wake namba moja,
Mimi huwa NIMEITRACK SIMU YA WIFE.
Hivyo nikaingia kwenye call zake, kwel nikakuta call ya mama yake wameongea kwa muda sana, nikadownload hayo maongezi, bahati mbaya yalikuwa kilugha chao na mimi sikielewi...
Nikamtumia rafiki yangu mmoja ambaye ni kabila sawa na wife hivyo akaitafsiri yale maongezi, yalikuwa hivi kiufupi
" Mama juzi nilivyoenda kulala kuna bundi alikuwa akilia hapa kwangu, na nilikemea akaondoka, ila nikapitiwa na usingizi mzito ambapo kuna ndoto ilinijia niko napigiwa ramri, na kuna sauti inaniambia wanamuita mumeo kwao kuna mambo anaenda kufanyiwa, moja ya anaemuita ni mama yake mzazi, nyumbani siyo kuzuri awe makini" mama yake akamuuliza umemwambia, wife akasema hapana, bhasi wakakubaliana wasiniambie ila waniombee tu Mungu aniepushe...
Wanajamvi, ninaomba ushauri wenu...mke hajui kama tayari ninajua alichoota, na pili kwa upande wangu siamini sana katika ushirikina, anaeweza tafsiri hiyo ndoto msaada jamani...
Mpaka sasa nimeahilisha safar zote nilizokuwa nimepanga.