Mwaka Wa Saba
Member
- May 27, 2020
- 29
- 38
Niende moja kwa moja kwenye mada yangu, Mimi ni kijana umri miaka 33.
Nimefanya kazi kama Mwalimu wa Sekondari kuanzia 2012 mpaka mwaka 2019 baada ya kupata fursa ya kwenda kujiendeleza kielimu nchini Marekani kuanzia January 2020.
Katika kipindi cha miaka hiyo 7 nikiwa kama Mwalimu nimepitia mambo ambayo mwanzo sikuwahi kuamini kama ni kweli au ni mapito madogo tu. Hapa nilihisi labda cheo changu kwani hapa nilibahatika kiukweli kuaminiwa na kuwa makamu katika taasisi kubwa mno na pia kusimamamia miradi mingi ambayo ilinisaidia kusafiri nchi mbalimbali. Nilijiona mwenye bahati na sijawahi kuwa tatizo kwa niliowaongoza.
Kwanza nilipoteza uoni wa jicho langu moja, pia kupata maumivu ya mwili mara kwa mara bila kujua chanzo chake hata pale nilipoenda hospital.
Nikiwa kazini nilianza kuandamwa na ajali japo sikuona ni tatizo kubwa katika maisha. Mwisho nikapata ajali mbaya nikiwa njiani kuelekea mkoani kuichukua familia yangu, kwa mapenzi ya Mungu nilitoka salama bila jeraha ila abiria niliokuwa nimewapa msaada walipata majeraha makubwa na wakaja kuzinduka baada ya mwezi.
Hapa nilipata mstuko kwani nilipelekwa mahakamani na kwa mshangao kesi ilichukua mwaka na nusu bila kuisha kwa madai wale majeruhi wanadai fidia na hapa nafikri polisi walijawa na tamaa ya hela.
Baada ya matukio hayo nikaaza kupata mitihani mizito tena, watoto wangu nao wakaanza kupata ajali za moto, kiasi kwamba muda mwingi nikautumia kwenye kuhangaika kutibu watoto na mimi mwenyewe.
Kitu kilichonisukuma kuandika hili ni hali ninayopitia baada ya kurejea Tanzania katikati ya mwaka 2020, Kila nilipojaribu kutafuta kazi ya kufanya nilijikuta mgonjwa, nikikaa nyumbani siiumwi kitu.
Nilijaribu kuacha kuhangaika kutafuta kazi hizi zinazohitaji taaluma yangu kwa hofu ya labda husda nijikite kwenye kazi ndogo ndogo kama kilimo, ufugaji au hata uvuvi, ila baada ya watu kuniona huko yanatokea mauzauza tena na lazima nipoteze kila kitu mpaka hata hela ya kula inaisha yote na hapo utapata taarifa watoto wanaumwa.
Kibaya zaidi nimetengwa na familia yote baada ya Mimi kugoma kujiingiza kwenye mambo ya kuamini kuwa nimerogwa, naweza amini hivyo ila sijaona kuwa suluhisho ni mimi kwenda kwa waganga.
Pia wengi wanaamini nimechanganyikiwa kutaka kufanya kazi kama kilimo au biashara ndogo wakifikiria nimetoka Marekani na nimesafiri sana iweje nisifanye kazi za ofisini kama akili ipo sawa? Binafsi hilo halinisumbui na sitaki kuamini kuwa lazima niwe ofisini kabisa.
Pia katika kipindi nikiwa vizuri nilikuwa na kundi kubwa mno la marafiki ambao nilijitoa kwao mno ila hapa ninaposema hata simu hazipokelewi labda wanahisi nataka kuwaomba hela. Hali hii imeniweka katika hali ngumu mno nisijue nianze na lipi nimalize na lipi.
Najaribu mno kutoka nilipo ila naanguka tena. Kwasasa ninaomba kama kuna mtu amepitia hali hii na alitokaje katika hili ajaribu kushauri, pia msaada mkubwa ninaoomba kwenu ni kama yupo mtu atahitaji tufanye kazi nitakuwa tayari huenda itasaidia mno, binafsi mwenyewe nahisi siwezi tena kwani hata mtaji wote umeteketea kwa kuilisha familia na matibabu wakati siingizi kitu.
Pia nitakuwa tayari hata kuishi porini kufanya kazi ili tu niokoe familia yangu.
Natanguliza shukrani zangu.