Msaada wa mawazo na ushauri, please only serious people here

Msaada wa mawazo na ushauri, please only serious people here

Najua hapa nazungumza na mzazi mwenye akili timamu,uzoefu wa maisha na anaeijua ndoa vizuri.
..
Ukumbuke kuwa kuna wanaume ambao ni watelekezaji hata kama wanaonekana wapo ktk familia.Sifa zao kubwa ni kubebesha mimba,kulaumu,Kukagua vyungu na kuishi kwa kutuhumu.Hawapendi kuambiwa ukweli hata ungekuwa mwepesi kiasi gani wakiambiwa hasira zao huzihamishia kwa mama,rafiki zake na watoto.Nina imani huyo ndiye mume uliyenae.Nini ufanye
...
SHIRIKISHA UPANDE WA MUME
Natambua wapo ndugu wa mume ambao wanakupenda na kukujali.Washirikishe suala lako,ukikwama nenda kwa wazee.Ambao pamoja na mambo mengine wanaweza kumuwekea utaratibu wa kutoa pesa toka pato lake au atafute kazi ili achangie matunzo ya watoto.
....
UTOFAUTI WA MILA
Uzoefu unaniambia kuwa bila shaka huyo mume mnatoka kabila tofauti hivyo kosa kubwa ulilofanya ni kumjengea utegemezi kwako tu pasipo kumpa nafasi ya u-baba uliokamilika (unless yuko frustrated na jambo fulani kwa muda mrefu) Sasa kutafuta talaka hakuna msaada kama utafikiria hivyo
....
NDOA YENU INA NGUZO MOJA
Wewe ndiye nguzo,,utakapojaribu kujitenga basi watoto,mali ulizojichumia zitazua mengine usiyotegemea.La muhimu ni wewe kama nguzo kusimama imara tena ikibidi kuweka sababu za kisheria kurudisha uwajibikaji ila kutengana hata kama huna hisia nae kimapenzi (result of unspoken dissatisfaction) hakutajenga.
...
MWISHO UMOJA KATIKA FAMILIA UNA GHARAMA.
Urudishe kwa busara,upendo,utaratibu na uangalifu wa hali ya juu.
Mungu asimame upande wako Mama.
^^
 
Mpige injili akishaokoka pombe kwa heri na kuwajibika ataanza........huko ndo kuvumiliana katika shida na raha.

umesema vema ndugu, huyo mpige Injili na kumwombea tena maombi ya kuatamia. Mungu ni mwema atamfungua ktk hivyo vifungo vya mwovu vya pombe. Kumwacha hiyo sio tiba nzuri kabisa na kamwe isitumike. Imeandikwa ''ndoa na iheshimiwe na watu wote'', pia imeandikwa ''alilo liunganisha Mungu mwanadamu asilitenganishe''. Mpende baba watoto wako, fanya toba kwa ajili yake, Mungu hatakutupa hilo ni jaribu tu.
 
mvumilie mpe muda wa mabadiliko kulea watoto peke yako tena matineja kuna changamoto nyingi sana usisubiri akutoe out one day panga wewe trip may be hata ya zanzibar mkaongee kwa kina natumaini suluhisho litapatikana tu kati yenu
 
Pole na uchovu , naamin unnatakiwa utumie busara katka maamuzi. Divorce inaweza ikawa ni chanzo cha matatizo mengine kama umeweza kumvumilia miaka 18 kwa nn iwe ghafla maana naamin we ndo umelea tatizo toka awali na huwezi kulibadili ghafla.
 
wapi huko jamani nami nimpeleke huyu wangu kwa delivernece? this is more than a burden to me now!!!!!
 
hapana hio siwezi. hio hela nibora nisave for my kids education. kubadilika hawezi kama hajabadilia for the last 18yrs how can he change now?? the change comes from himself and if he doesnt see why he should change maybe that is the reason he is behaving that way. anyway thanks for your advise but the problem is i have no love for him at all any more!!!! hapo ndio shida kubwa ilipo.watoto atawalea saa ngapi Neddy wakati anakuja usiku wa manane tena siku nikisafiri ndio anarudi asubuhi. you cant imagine......
 
Himidini nashukuru sana na wote mliochangia mada. ni kweli inaonekana nimelea mm hili tatizo ila ni sababu i wanted the best for our kids and our home. mimi ni mwanamke wa kihaya nisiokubali umaskini hata kdg ndani kwangu. napigana na kufanya kazi kwa bidii sana. nimeshawashilikiza wazazi wa pande zote mbili na hata wazamini wa ndoa. wote wanalijua hilo na wanamjua fika kijana wao ni wa namna gani. he is a kind of ignorance he dont care hurting you at all....unyumba wenyewe naweza hata kaa mwezi hatujagusana. sababu kila mara anarudi usiku wa manane. ni mfanya bishara its not easy to control his income. nadhani ni mila ndio zinamsumbua i really dont know. yaani wapendwa nimechoka mpaka bac. nimevumilia mpaka sasa hv nina vidonda vya tumbo na pressure ya kushuka. nawaa bila majibu.nifanyeje sijui. ndio maana nikaona nililete hapa kwenu. returning the love back is not easy coz i just dnt love him anymore kwa yale yote anayonifanyia.
 
mvumilie mpe muda wa mabadiliko kulea watoto peke yako tena matineja kuna changamoto nyingi sana usisubiri akutoe out one day panga wewe trip may be hata ya zanzibar mkaongee kwa kina natumaini suluhisho litapatikana tu kati yenu

hao watoto nawaleaga mimi mwenywe Neddy bila msaada wake kama anaondoka asbh na kurudi usiku anawalea saa ngapi. infact namshukuru Mungu watoto wangu wanaelewa kila kitu and i talk to them everyday. ni wasikivu sana kwa kweli. ni kweli mimi ndio nimelea hilo tatizo sio siri ila utajikaushaje wakati unaona mtoto wako karudishwa ada siku ya kwanza ya pili na una hela? itabidi ukalipe tu. au hamna chakula na wala hajali wala hanunui mtalala na njaa wakati una hela? itabidi ukanunue tu chakula mle mlale... kwa hio ndio hv
 
Pole sana dada kokuemage
Mi nadhani uongee na hao friends wake ... kuna watu hawana msimamo wao ni rahisi sana kufata influence ya friends
sasa kama jamaa yeye ni pombe tu ... am sure he doesnt go out peke yake.

kama hapatikani usiku basi make time ya kuongea nae kila siku asubuhi during breakfast kabla hajapiga mitungi
 
We rafiki hapana sumbua semeji, ila sista umevumilia miaka 18, kwani usiendelee?? Huenda akabadilika
 
du sasa hapo katika uvivu na ulevi ndiyo taabu ya wamasai, ila we fanya unavyoona ni vyema maana mimi Biblia inaniambia "ndoa na iheshimiwe na kila mtu" na pia inasema "..alichokiunganisha Mungu, mwanadamu hawezi kukitenganisha" mpaka hapo naona naeleweka kwa nini sishauri kuachana kwa hawa ndugu
Mimi ni mwanamke nina miaka 37 sasa hivi,nimeolewa na nina watoto watatu miaka 17,13 & 6yrs.Nimeishi na mume wangu kwa miaka 18 sasa hivi,mume wangu ni maasai wa mjini sio wale wavaa lubega.

Tatizo ni huyu baba nimembeba sana mpaka naona nimechoka na vile umri umeenda sijui nifanyeje. Sio mwanaume muwajibikaji kabisa.

Hajui ada za wattoo zinatoka wapi, chakula, maendeleo ndani ya nyumba, hajui chochote yeye ni kama mtallii.Hata akiona pazia liko upande hatengenezi au chumba hakina bulb hajigusi, ni mimi ndio nifanye.

Ada za watoto ndio kabisa akijatahidi sana kama ada ni laki 4 basi atatoa laki 2 tena kwa shida na kwa awamu. Akikuta hela zako au pochi umeweka vibaya anaruka mpaka na hela zako.

Sio muwajibakaji hata tone yeye ni starehe na starehe na yeye.

Kweli nimevumilia sana tokea mwanzo ila mbona naona kama siwezi tena? mzigo umenilemea na hana msaada wewe ndio ukimbizane watoto watakula nini, watasomaje, watavaa nini, nyumba inaitaji nini etc.

Ndoa ni kwa shida na raha,nimejenga nyumba mwenywe na kila kitu nimefanya mwenywe tena yeye ulikuwa ukimpa hela ndio anaenda kulewa, mpaka leo ana miaka 43 sasa hivi ni wa kurudi usiku wa manane.

Nimechoka kuvumilia jamani namuambia aondoke aniache maana nyumba ni ya watoto na ni nguvu yangu, mwenywe hataki.

Ukipika chakula akikuta anakula hajui hata kinatoka wapi.

Juhudi zote za maendeleo na watoto ni mimi mwenywe.

Haya maisha yamenichosha sana jamani nifanyeje nimejikuta simpendi tena kabisa na sina hamu nae kabisa hata ya mapenzi.

Sina mpenzi wa nje basi tu nimeona huu ni mzigo ambao umefika mwisho,nataka nimuche nafanyaje na yeye ndio amekataa kutoka ndani ya nyumba kabisa? nimechoka kweli kwei.

Toka kanioa ni ile miezi ya awali ndio alishawahi nitoa out,sikumbuki hata mara ya lmwisho aliniambia mke wangu twende out ni lini, au tukakaa kupanga maisha/maendeleo ya watoto au chochote ni lini.

Mimi ndio wa kukimbizana na maendeleo ya shule ya watoto. Kila siku ni kuomba kulipa ada kwa instalment.

Nimekua ndio kama niko peke yangu yeye akija usiku na mtungi wake ni kelele na kulala.

Yuko kama vile anaishi guest,akija usiku saa zingine fujo na kelele. Sikumbuki hata mara ya mwisho ameshawahi nipa laki ya matumizi au hata elfu 50 ni lini? akitoa hela ya chakula ni elfu 20 kama mara ya mwisho kanipa miezi 2 iliyopita.

Hata nikiwa na msiba kwetu hakanyagi wala haudhurii.

Jamani hebu nishaurini nifanyeje?
 
Thread hii iwe fundisho kwa wale wote wanaoingia kwenye ndoa wakiwa na mawazo "atabadilika tu huko mbeleni" au "nitajitahidi nimbadilishe tu"...wakati wakisema hayo mioyo yao inakuwa imejaa furaha kwa kuwa wamepata mwanamke mwenye shepu nzuri au mwanaume hendisamu.

Dada pole sana ila hujachelewa Mungu bado yupo na nira yake ni laini.
 
Himidini nashukuru sana na wote mliochangia mada. ni kweli inaonekana nimelea mm hili tatizo ila ni sababu i wanted the best for our kids and our home. mimi ni mwanamke wa kihaya nisiokubali umaskini hata kdg ndani kwangu. napigana na kufanya kazi kwa bidii sana. nimeshawashilikiza wazazi wa pande zote mbili na hata wazamini wa ndoa. wote wanalijua hilo na wanamjua fika kijana wao ni wa namna gani. he is a kind of ignorance he dont care hurting you at all....unyumba wenyewe naweza hata kaa mwezi hatujagusana. sababu kila mara anarudi usiku wa manane. ni mfanya bishara its not easy to control his income. nadhani ni mila ndio zinamsumbua i really dont know. yaani wapendwa nimechoka mpaka bac. nimevumilia mpaka sasa hv nina vidonda vya tumbo na pressure ya kushuka. nawaa bila majibu.nifanyeje sijui. ndio maana nikaona nililete hapa kwenu. returning the love back is not easy coz i just dnt love him anymore kwa yale yote anayonifanyia.

^^
Kwanza hongera kwa ustahimilivu ambao kweli ni wachache wanaoweza kufika hapo ulipofika.
..
Pili, Bado kikwazo kikubwa ni hatima ya watoto kuishi pande mbili ilihali wazazi wote mpo hai.Kwa kuwa ndugu zake wanajua mwenendo wake basi usimuonee aibu kwa kuchukua hatua za kifamilia,na kama unaogopa utaharibu mahusiano ya ndani ni vema ukatumia wazee wachache ili kumfanya awajibike.
..
Tatu
Kufikia hatua ya mwezi bila kukutana ktk unyumba ni hatari nyingine inayofukuza mawasiliano nje ya nyumba yenu. Hili huwapata wanawake wengi unaweza kutumia indirect way kujua wengne walilitatua vipi,ukiona njia inafaa basi uitumie.
..
Nne
Pole kwa presha na magonjwa mengine yanayokuandama ikiwa ni matokeo ya msongo wa mawazo.Miaka kadhaa nilikuwa ktk shirika la Partage huko Bukoba,Katika kuzunguka mle migombani kwa kazi za kiofsi kuna Mzungu incharge wa eneo letu alinionesha mmea fulani unaitwa 'entula' (kwa lugha ya kihaya ntasahihishwa kama nimekosea) unatoa matunda fulani madogo ni machungu kiasi,huwekwa juu ya ndizi wakati wa mapishi.. Tumia sana na mara kwa mara husaidia sana kupunguza presha.
..
Pole Mama,, huu si wakati wa kujihukumu kupita kiasi wala kutafuta wa kulaumu. Bali ni wakati wa kutazama unasimamia vipi nia yako ya kuwa na familia imara..
Hufika mahali ktk Maisha tunahitaji kufanya tu kana kwamba mwenzetu hakuwahi kuwepo
^^
 
Huyo ndio MUMEO na sijui unatafuta ushauri wa namna gani wakati ushakuwa na maamuzi ya kumwacha.Binadamu wote hawako sawa Shemeji,kumbuka huyu mtu kakuzalisha watoto 3,huoni kama watoto utawahuzunisha? Usidhani na watoto hawampendi kama wewe! chunga ndoa yako Mungu atakubariki kupitia wema wako kwa mmeo huyo.ni Pm nikupe ushauri.
 
Pole sana dada kokuemage
Mi nadhani uongee na hao friends wake ... kuna watu hawana msimamo wao ni rahisi sana kufata influence ya friends
sasa kama jamaa yeye ni pombe tu ... am sure he doesnt go out peke yake.

kama hapatikani usiku basi make time ya kuongea nae kila siku asubuhi during breakfast kabla hajapiga mitungi

Thanks Sita ila ni ngumu coz yeye anarudi mmeshalala kuamka mimi nimeajiriwa lazima saa 12 niwe macho kwa ajili ya kwenda kazini yeye ndio kwanza anakoroma anakusubiria ukishaondoka ndio aamke. mara chache sana tunawa wote nyumbani. nimeshaongea nae sana mpaka na marafiki zake wote wanasikitika hivo hivo ila habadiliki sijui kwa nn. Watu8 ni kweli never marry a man expecting him to change. hii na iwe fundisho kwa watu wote ambao hawajoa/kuolewa. Nadhani na yeye hana msimamo pia.
 
Kwa kweli siwezi kumhukumu ila ni kuomba Mungu aweze kubadilika.
Unajua ingekua rahisi kama mtu anamwogopa Mungu.... lakini huyo Maasai anaonekana ni Kiburi kunizidi mimi.
Hapo mlipo tayari mpo separated ka sababu u dont share anything together apart from the bed.

Kuna mtu aliwahi kutoa ushauri kwenye post moja akasema dawa ni kumfanya awe na wivu. Siku moja na wewe jipige makeup alaf utoke usiku (just go anywhere) wakati yeye ndo anarudi. Hakuna mwanaume anayeweza kuvumilia kumwona mkewe anatoka usiku. Lazma roho iruke... ila be careful maana kama hatojali ndo utakua umeanzisha drama nyingine
 
umesema vema ndugu, huyo mpige Injili na kumwombea tena maombi ya kuatamia. Mungu ni mwema atamfungua ktk hivyo vifungo vya mwovu vya pombe. Kumwacha hiyo sio tiba nzuri kabisa na kamwe isitumike. Imeandikwa ''ndoa na iheshimiwe na watu wote'', pia imeandikwa ''alilo liunganisha Mungu mwanadamu asilitenganishe''. Mpende baba watoto wako, fanya toba kwa ajili yake, Mungu hatakutupa hilo ni jaribu tu.

tehetehe maombi ya kuatamia mpaka yai linatotolewa nimpenda hiyo.
 
Back
Top Bottom