Msaada wa mawazo: Mwenye ufahamu wa biashara Malawi na Rwanda

SANGA ONE

Senior Member
Jul 7, 2012
125
28
Habarini wana jamvi ,
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza naomba kusaidiwa kimawazo.
Nilienda kwa ndugu yangu kumuomba anikopeshe fedha kwa ajili ya mtaji lakini kinyume na matarajio yangu, ndugu yangu huyo alinijibu mimi hela ya kukupa sina ila naweza kukufundisha jinsi ya kupata pesa.

Ameenda mbali zaidi na kuniambia miaka miwili nyuma alikuwa anafanya biashara ya pembejeo za kilimo na kuzipeleka sehemu mbali mbali za Malawi na Rwanda Hivyo kaniambia kama nipo tayari nikatafute masoko kisha yeye atanipa mzigo nikauze nipate hela ya mtaji. Wadau sijawahi kwenda Malawi wala Rwanda so sijui hata pa kuanzia.

Huyu ndugu yangu huwa analeta kontena toka China za bidhaa za kilimo kama madawa, bomba za kumwagilia mimea nk, mwenye uzoefu naomba anipe japo mwanga kwani brother kagoma kabisa kunipa cash asanteni na karibuni kwa mawazo.
 
Back
Top Bottom