Msaada wa maombi mazito, Mama anaangamia!

Secret Star

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,720
1,639
Habari jamani,

Naombeni sana msaada wenu JF kwa mwenye ujua juu ya hili nina mama, anasumbuliwa sana na maradhi ya mgongo na na chembe ya moyo. Hospitali tumeshindwa.

Msaada wa maombi ndugu zangu kwani hata kulala wala kutembea hawezi..
 
Habari jamani, naombeni sana msaada wenu JF kwa mwenye ujua juu ya hili nina mama, anasumbuliwa sana na maradhi ya mgongo na na chembe ya moyo, Hospitali tumeshindwa msaada wa maombi ndugu zangu kwani hata kulala wala kutembea hawezi..
Pole sana mkuu...kama vp mpeleke makanisani akaombewe
 
Maskini pole sana mungu atampa mama nafuu jaribu na dawa za kiarabu na kihindi huwa zina msaada sana naimani zitampa nafuu mama.pole sana
 
Atapona tu. Hakuna ugonjwa au udhaifu unaoshindikana kwa Yesu. Biblia inasema "Yote yawezekana kwake aaminiye". So hatua ya kwanza ya kupokea uponyaji ni kuamini kuwa Yesu anaweza kuponya.

Injili zote kuanzia ile ya Mathayo hadi Yohana, Biblia imejaa shuhuda ya matendo makuu ya uponyaji Bwana aliyotenda akizunguka huko na huko kutangaza Habari za Ufalme wa Mungu.

Ona alivyomponya mtu mwenye ukoma kwenye Mathayo 8:1-4. Lakini kama hiyo haitoshi, Yesu alimponya mtu mwenye ugonjwa wa kupooza bila hata kuonana naye. Hii ni baada ya kupewa taarifa na boss wa huyo mtu na Yesu alipoiona imani ya huyo boss pale pale akaagiza uponyaji na yule mtu akapokea uponyaji instantly. Hii tunaiona kwenye Mathayo 8: 5-13.

Mifano ipo mingi sana ya nguvu ya uponyaji wa Yesu. Angalia jinsi alivyomponya mwanamke aliyekuwa akitoka damu kwa muda wa miaka 12. Mwanamke huyu alipokea uponyaji wake kwa kugusa upindo wa vazi la Yesu. Imagine that! Yaani hadi mavazi ya Yesu yana nguvu! Hadithi yake utaiona katika Mathayo 9:20-23. Mfano mwingine tunauona kwenye Luka 5:17-20 ambapo watu wanne wanamleta rafiki yao aliyekuwa ameparalyze. Yesu ipoiona imani yao tu, akaagiza uponyaji na yule mgonjwa akainuka instantly.

Tunaweza tukaendelea tena na tena juu ya mifano kama hiyo ambayo Yesu alitenda kwa wagonjwa na wenye udhaifu. Ni mingi sana hatuwezi kuimaliza lakini kitu cha muhimu kabla ya kupokea uponyaji wako ni kuwa na IMANI. Imani ndiyo daraja linalokuunganisha kati yako wewe na uponyaji wa mama yako. Huna haja ya kupanic wala kubabaika. Nguvu ileile iliyotumika kuponya enzi zile za Yesu ndiyo hiyohiyo itakayotumika kumponya mama yako siku ya LEO. Yes, namaanisha LEO HII.

Sasa niruhusu niombe kwa ajili ya mama yako.

"BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI. KAMA AMBAVYO NENO LAKO LIMESEMA KATIKA ISAYA 53:5 KUWA KWA KUPIGWA KWAKO SISI TUMEPONA, NAAGIZA NGUVU YA UPONYAJI SAA HII NA DAKIKA HII KWA HUYU MAMA NA KUANZIA SASA AWE MZIMA KWA JINA LA YESU KRISTO MWANA WA MUNGU ALIYE HAI. AWEZE SASA KUINUKA NA KURUDISHIWA NGUVU NA AFYA YAKE KAMA ZAMANI. AMEN.

Mama yako ameshapokea uzima kupitia maombi haya. Ni kama utani tu, lakini ndiyo imeshatendeka. Kama upo naye karibu jaribu kumwambia afanye vitu ambavyo alikuwa hawezi kufanya na UTASHANGAA kuona mabadiliko makubwa sana. Usisite kuandika ushuhuda wako na kuupost hapahapa JF ili tuwatie moyo watu wengine wenye matatizo kama yako. Lakini muhimu kuliko yote, ufanye bidii kutafuta kanisa lililo karibu nawe ambalo linahubiri habari za Yesu Kristo. Hapo wewe na mama mtapata mafundisho ya kuwajenga imani yenu kwaajili ya SAFARI YA KWENDA MBINGUNI. Hilo ndilo muhimu kuliko yote.

Mungu awabariki
 
Asante sana ndugu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom