yaani wewe acha tu
ila ukikuana na mhubiri wa kweli anakuambia, kila mtu chanzo cha tatizo lake huwa analijua.
Mimi nialike tu kukusaidia kuomba, lakini ni jukumu lako kujiombea maana tumepewa nguvu sawa wote.
Alichosema ni hiki, watu wanakimbilia kuombewa wakati hata Mungu wanayemuomba hawamjui ni Mungu yupi.
Akawa anasema, Mungu wangu si lazima awe wako, japo wote tunatumia bibilia moja.
Cha kwanza, jua unamtumikia Mungu gani, ndio uombe, na uwaalike wengine waombe pamoja nawe.
Mtu anaenda kuombewa, kumbe tatizo lake liko kwenye ukoo, mchungaji atakusaidia nini??
Au mtu anaombewa maisha yaboreke, wakati ni mvivu au mfujaji wa mali?
Mtu ananeda aombewe ana mapepo wakati kutwa kucha kwa waganga? Na labda keshafunga nao agano?
Akawa anasema, mtu na ajiombee mwenyewe tu, wengine watamsaidia lakini hawawezi ondoa tatizo lake.
Hahaha,
Father of All, hata bible imeandika. Wataweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya. Wakati mwingine mtu wala hahitaji maombi, zaidi anahitaji counselling.
I have my reservations kuhusu nabii flora and some famous pastors though, maana focus ni juu yao na sio Bwana mtoa uzima. Maombezi hayapashwi.kuwa kama uganga wa kienyeji, kuwa asipokuwepo mwenyewe hayafanyiki.