Pole yake.
Natumia OPPO toka kipindi cha awali zitoke Tu. Bahati mbaya kabla hata sijamaliza siku mbili toka kuitumia,nikaweka password mfano buda2019 kumbe wakati wa kuweka na kuthibitisha password niliweka buda209. Kwa hiyo password kumbe ulikuwa buda209 na siyo buda2019.
Na siku hiyo nilinunua simu yangu na kuelekea home baada ya shughuli iliyonipeleka mjini kuisha, nikarudi zangu Shinyanga .
Dah,nikaulizia pale shinyanga wapi wanaflash simu, wakasema sijui Kwa mchina, mchina akashindwa.
Baadae ikawa inakuja text kuwa niwaone oppo Kwa msaada.
Ikabidi nirudi dar baada ya mwezi mmoja maana nilikuwa kikazi tena pande zile. Nikaenda pale nilipouziwa,wakasema hawana msaada wowote isipokuwa oppo wenyewe, nikaelekea ofisi zao pale posta,wakanisaidia kuiondoa
Ila sharti uwe na kasha la simu uliyonunulia na uwe na risiti ya manunuzi .
Hizi simu za hawa jamaa ziko protected Sana.
Huwezi ku flash mtaani