Msaada wa kufika Mafia kisiwani kutokea Dar

lydiah

Senior Member
Sep 2, 2015
151
101
Habari zenu wakuu...
Eti nauliza ni njia gan rahisi kufika mafia kutokea Dar es Salaam? Maana wengine wananambia nipite mbadala wengine kigamboni sasa sielew which is which... Na vipi Kuna uwezekano wa kwenda kwa ndege?
Naomben msaada wenu wenyej wa huko
 
Inabidi uende kwa ndege kwa usalama wako. Nilishawahi kwenda Mafia kwa kujifanya mtu wa adventure nikapanda bus mpaka mbagala rangi 3 Dar es salaam,halafu nikapanda hiace mpaka Nyamisati. Nyamisati nikalala guest ya elf 10 na mji mzima ulikua giza si mchezo, kesho yake asubuhi nikapanda boti mpaka Mafia. Kwa jinsi ilivyojaa na maji yalivyokua yanaingia ndani nikasema siwezi rudi na boti tena. Niliinyoy anyway ila wakati narudi nilipanda ndege ndogo hizi ilikua kama laki na kitu shirika linaitwa Tropical Air.

Natumai umesikia huko Nyamisati kibiti jamaa wameua raia kwa risasi juzi. Kibiti saga.
 
ni vyema upande ndege kama uchumi unaruhusu ni laki na ishirini kwenda na pia itakuwa ni bora kwa usalama wko,, ukisema upande basi kwanza njia yenyew na mvua zile zilivyinyesha cjui ipoje halafu pia usalama ni mdogo mnaweza mkakutana nao jamaa wale wa kibiti
 
Back
Top Bottom