Msaada wa ku trade iphone x

Msaada wa ku trade iphone x

Issuna

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,204
Reaction score
7,648
Nina iphone X katika matumizi matumizi mwezi ulopita nili ilaliaje sijui ki ukweli ila nimeamka asubuhi nashika SIMUnakuta display ni white blank,hamna maandishi kioo kinawaka kama tubelight ule mwanga wakucheza cheza.

Nikadhani tatizo litaisha baada ya muda ila halikuisha na baadae nikaamua kuibadilisha kwa kumtuma ndugu yangu anae enda DUBAI anunue kioo huko then abadilishe so nikaokoka na cost za usafiri wa mimi kwenda au ituma simu,cost yake ili cost 530,000 simu kweli ikarudi like new.

Jana katoto kangu kaliskia simu inaita kakaibeba kakawa kananletea,kakiwa koridoni simu ikamponyoka ikadondoka,kakaiacha pale pale kakaja nifata nambia simu imedondoka,naifata naikuta na majanga yale yale yalonkuta mwanzo,simu inaendelea kuita ila Screen nyeupeee yani nimechanganyikiwa hapa sitamani tena itengeneza hii simu.

Nimeingia website ya APPLE nataka kununua XR NIACHANE na hiii pasua kichwa nimeona Kitu ambacho ndio kimenifanya nifungue hii THREAD hapa,katika manunuzi pale kuna option mbili

1.Kulipia amount inayohitajika kupata simu husika
2.Kufanya Trade ya simu uliyonayo ya IPHONE then unaongezea hela kidogo wanakupa nyingine

Kuna vipengele vya kujaza pale vya aina ya simu,storage,colour,nk sasa swali langu na ombi langu ni kusaidiwa kufanya hii kitu maana ki ukweli sijawahi fanya hii kitu..nataka kutumia OPTION no.2 ya kurudisha hii X yangu then niongezee amount watayohitaji niweze pata simu ingine Mpya.

Process hii sijajua ni ya USA tu au hata huku kwetu tunaweza TRADE simu zetu...kwa yeyote anaeweza fanya hiii kitu Naomba anisaidie najua atatumia muda wake na bando lake katika kufanikisha hili na kujua details za kila kitu so NITAMLIPA (sio bure)

Yeyote anaeweza nisaidia hiki kitu nikaweza rudisha hii simu then nikaongeza hela nikapata Simu ingine NITAMLIPA AMOUNT ATAYOHITAJI YEYE NIMPE....nipo serious undefined% kwa mwenye solution ya ombi langu.

Kuna mtu kanambia KENYA wanabadili yani wana TRADE an old iphone then una top up wanakupa NEW phone kulingana na condition ya SIMU yako.

Name : iPhone X
Storage: 256GB
Colour: White

Mwl.RCT na wengine wote nisio wafahamu naombeni msaada wenu,ndugu yenu natumia simu sioni anaepiga yani kibubu bubu.

MREJESHO:

Hatimae Jana nimefanikiwa kupata kioo na msaada ni wa member wa humu humu JF,nashukuru sana mkuu na kuna member mwngine aliejaribu nisaidia mwenye namba inaishia 477 nashukuru sana kiongozi kwani niliahidi nikishindwana na huko ninapoenda ningerudi kwako,bahati mbaya sikukutafuta kwenye simu kukupa mrejesho(samahani kwahilo)

This time around JF imeokoa Amount kubwa sana...asante zaidi kwa brother Maxence Melo Mike Mushi nyie watu mmeturahisishia sana maisha..asanteni sana!
 
Daah kweli tunatofautiana guyz! Sie wa Tecno na Huawei tumejiona kama tuko kwenye chumba cha mtihani! Yaani hatuelewi kitu kama kutrade kinatuhsu!
 
mkuu si utafute tafute zenye icloud kwanza utapata hata kwa 300k.hata akuuzie kioo tu.
 
Msichofahamu ni kuwa kuna iphone fake nyingi zipo sokoni lakini ukiiangalia ni kama yenyewe kabisa kwa kila kitu
 
Hakuna simu rahisi kujua kama ni fake kama iphone wataiga shape na vitu vingine lakini ios itawaumbua na huduma zake mama icloud. Mtu ambaye anaweza pigwa iphone fake ni yule ambaye hajawahi tumia iphone kabisa.
 
Sawa
 
Na sio kuitumia tu yaani huyo atakua ni ndezi kabisa hajui chochote sehem yeyote ile .iPhone itabaki na utofauti wake kinachonipaga taabu huko ni ukomavu wa store yao ,utunzaji wa chaji na pia matumizi mengine madogo madogo ambayo hayana uwiano na ukomavu wa ulimwengu wetu wa tatu
 
mkuu si utafute tafute zenye icloud kwanza utapata hata kwa 300k.hata akuuzie kioo tu.
nimetafuta nikawapa kazi mafundi wameshndwa wote wanaendeshawe na TAMAA wabongo wakishajua unataka kiooo wanaropoka tu bei..

Kuna mtu kancheki muda si mrefu kanambia anipe kiooo ila anataka 1.5M unaweza imagine mkuu.
 
Hakuna simu rahisi kujua kama ni fake kama iphone wataiga shape na vitu vingine lakini ios itawaumbua na huduma zake mama icloud. Mtu ambaye anaweza pigwa iphone fake ni yule ambaye hajawahi tumia iphone kabisa.
upo sahihi chief..kwa asilimia kubwa
 
Jibu ni hivi, ama ununue simu mpya aina hiyo au ununue aina nyingine.
Kuhusu replacement ya kulipia kidogo inawezekana tu, kama simu yako ilikuwa na insurance. Kama ungekuwa umeiwekea insurance unaipigia insurance campany inayohusika, kisha wanahakiki taarifa zako, na hicho kiasi kidogo unachokingelea ni dedactable amount unayolipia ili insurance i process replacement ya simu yako, amount anatofautiana kulingana na thamani ya simu husika inaweza kuwa $200 au $500. Na unawatumia hiyo simu iliyo haribika wao hukutumia replacement.
Lakini mara nyingi hawakupi simu mpya, hukupa refabrished phone, itafanana kwa type na model na yako lakini isiwe exactly the same, hapa sijui nikuelezeje but ndio hivyo, inaweza kuwa mbaya kuliko hata hiyo uliyo nayo but that is refubrished phone na ndivyo replacement hufanyika. Unakuta mwingine aliirudisha inamatatizo labda kama yako au tofauti, wao wanaikarabati inafanya kazi kisha unapewa wewe. Hivyo ndivyo nafahamu kuhusu hii issue yako kutatua tatizo lako la simu uliyo nayo.
Sina uhakika kama hapa nyumbani tuna lipia simu kidogo kidogo yani mortgage finance, simu kama marekani. Kule unalipia kidogo kidogo principal, interest, data service na insurance, sasa inapo haribika au kupotea ndio insurance ina replace, baada ya kulipia dedactable na wanakutumia hiyo replacement.
 
mkuu si utafute tafute zenye icloud kwanza utapata hata kwa 300k.hata akuuzie kioo tu.
nitafutie mkuu yenye icloud tuchomoe kiooo..ikipatikana kwa 300k nakuahidi nusu yake 150k nakupa wewe

Naomba uje pm kama utafanikisha hilo.
 
Jibu ni hivi, ama ununue simu mpya aina hiyo au ununue aina nyingine.
Kuhusu replacement ya kulipia kidogo inawezekana tu, kama simu yako ilikuwa na insurance. Kama ungekuwa umeiwekea insurance unaipigia insurance campany inayohusika, kisha wanahakiki taarifa zako, na hicho kiasi kidogo unachokingelea ni dedactable amount unayolipia ili insurance i process replacement ya simu yako, amount anatofautiana kulingana na thamani ya simu husika inaweza kuwa $200 au $500. Na unawatumia hiyo simu iliyo haribika wao hukutumia replacement.
Lakini mara nyingi hawakupi simu mpya, hukupa refabrished phone, itafanana kwa type na model na yako lakini isiwe exactly the same, hapa sijui nikuelezeje but ndio hivyo, inaweza kuwa mbaya kuliko hata hiyo uliyo nayo but that is refubrished phone na ndivyo replacement hufanyika. Unakuta mwingine aliirudisha inamatatizo labda kama yako au tofauti, wao wanaikarabati inafanya kazi kisha unapewa wewe. Hivyo ndivyo nafahamu kuhusu hii issue yako kutatua tatizo lako la simu uliyo nayo.
Sina uhakika kama hapa nyumbani tuna lipia simu kidogo kidogo yani mortgage finance, simu kama marekani. Kule unalipia kidogo kidogo principal, interest, data service na insurance, sasa inapo haribika au kupotea ndio insurance ina replace, baada ya kulipia dedactable na wanakutumia hiyo replacement.
Screenshot_1.png

Mkuu hii wanayosema kwenye website yao ina maana haituhusu sisi wengine au nakua sijakuelewa?
 
nimetafuta nikawapa kazi mafundi wameshndwa wote wanaendeshawe na TAMAA wabongo wakishajua unataka kiooo wanaropoka tu bei..

Kuna mtu kancheki muda si mrefu kanambia anipe kiooo ila anataka 1.5M unaweza imagine mkuu.
qumamae kisa kasikia ni iphonex,si atoe sasa hiyo lock ndio auze kam anayo marinda pumbaavu.
 
Back
Top Bottom