Msaada wa kisheria, nataka kuachana na mke wangu

Stunted

Member
Jul 5, 2014
30
9
Msaada wa kisheria, nataka kuachana na mke wangu.

Habarini za weekend magwiji wa sheria. Mimi ninaishi na mke wangu (bila ndoa kwani ni dini tofauti) kwa takribani miaka 4. Huyu binti sikuwahi kumpenda japo yeye alinipenda sikutaka kujiingiza kwenye penzi kwani nilijua kuoana itakuwa ngumu, na wala sikutaka kufanyanaye mapenzi kwani sikuwa na nia ya kumchezea. Yeye alisisitiza tufanye hatakama sitamuoa. Kwa bahati mbaya au nzuri siku tumefanya na mimba ikaingia, sikutaka kukubali kirahisi kwani sikuwa na uhakika kama ni kweli mimba ni yangu. Baada ya kujifungua niliona mtoto anafanana nami hivyo kuamua kuishi naye hadi leo.

Kwanini nataka kumuacha

Tangu tuishi wote ndoa imekuwa ni ya misukosuko mno, mwanamke kajaa kiburi na dharau chungu nzima, hapendi ndugu zangu, mkigombana kidogo anaenda polisi ama Ustawi wa jamii, ni mshali kupita kiasi, hapendi kuomba msamha na kukiri kosa.
Kutokana na hali hiyo ilinichukua muda mrefu kutangaza ndoa japo yeye alikubali kuingia ukristo. Sasa anadai alikuwa ananipenda zamani kwa sasa ni kawaida tu, pia wazazi wangu hawajakubaliana nifunge ndoa naye kwani kwa Tania alizo nazo anaweza kutaka tuachane na Mimi nimefunga ndoa ya kanisani yeye anaweza achika na akafunga ndoa nyingine.

Sasa nataka kumuacha, tumejenga nyumba na tu na Mtoto mmoja. Nini hatima ya nyumba yetu na mwanangu endapo tutaachana?? Mtoto ama miaka 3.

Naombeni ushauri wa kitaalamu.
 
Shida umezikaribisha mwenyewe... Toka mwanzo ulishaona daili ya mahusiano yenu siyo mazuri... Uliashaona mwanzo mbaya na mwisho wake utakuwa mbaya.. Lakini ukaamua kuyachukulia kirahisi...
 
Acha kulialia boss.....kwani nyumba ina vyumba vingapi? Gawaneni vyumba kisheria tena wahi chenye masterbedroom ili ukija na mzigo mwingine usisumbuke kupita pita cordoni........mtoto ataishi sebukeni paka apo baadae man sebuleni itakua katikati hapo kila mtu atakuwa na uhuru wa kumuona.
Fuatilia kwa maanani ushauri wangu.
 
Kigezo cha kuishi na mwanamke kwa kipindi fulani pamoja bila ndoa kitakubana Mkuu na itahalalishwa ndoa kamili hata kama hamjafunga ndoa . Kuhusu kugawana nyumba mahakama itaamua baada ya kuridhishwa na mchango wake katika ujengaji wa nyumba hiyo .
 
Asante mkuu kwa mchango
 
That moment when i think of marriage na stor kaa hz utokea naamua kutuliza miguu...vnakatshana tamaa
 
mmmhhh pole sana bt ukikaa na mwanamke mwaka mmoja kisheria ni mkeo, na pia mkiachana mtagawana mlivovuna pamoja,na mtoto atakuwa upande wa mama mpaka akifikia miaka 7.
 
Kwa sasa bado naishi naye japo hatusemeshani, je naweza mpa talaka?? Kwaharaka haraka hawezi kukubali kutoka kwenye nyumba.
Uumpe talaka kwani mumeoana? Huyo kama muislam harothi chochote kwa imani yake maana si mkeo a wewe pia huyo mtoto kama ungekuwa muislam asingepaswa kukurithi maana si wa ndani ya ndoa labda umpe mali kama za wadi kabla ujafa na kama wazee wa bint wako strict mtoto si wako pia ni wa mama tu!
Inshort huyo bibie si mkeo ila kama ana nguvu zake katika mali hiyo kesi nyingine kinyume cha hapo mya deal na matunzo ya mtoto au rithisha mtoto nyumba!
 
mmmhhh pole sana bt ukikaa na mwanamke mwaka mmoja kisheria ni mkeo, na pia mkiachana mtagawana mlivovuna pamoja,na mtoto atakuwa upande wa mama mpaka akifikia miaka 7.
Sio mwaka mmoja ni miaka miwili (miezi 24 mfululizo chini ya paa moja). Hii haiji tu automatically ni mpaka mahakama iamue kwamba kweli kulikuwa na "fikirio la ndoa" pale watu hawa wanapoamua kuachana.
 
Mkubwa sheria inavigezo vyake mpaka umpe mtu talaka, na mahakama haipo kwa ajili ya kutenganisha ndoa, cha msingi tengeneza saikolojia yako kama kweli we n mkristo hlo swala mbna dogo sana lipeleke msalabani, au ukiona taabu sana kwa maana unataka msaada wa kisheria kwa wakili unalipiwa, so kwa kukusaidia kabla hjawaza kuachana hebu jarbu kumwona jamaa moja anatiwa Mr Mauki au aunt Sadaka atakusaidia kisaikolojia.
 
That moment when i think of marriage na stor kaa hz utokea naamua kutuliza miguu...vnakatshana tamaa
Kila mtu na ndoa yake,usijifananishe na watu wengine DNA yako ni tofaut na destiny yako ni tofauti.chukua hyo
 
Umepewa ushauri mzuri sana kuanzia kulala vyumba tofauti hadi kupeleka tatizo 'msalabani'...
Vyoote hivyo vikishindikana, chukua mkopo (kwa siri) kupitia hiyo nyumba...alafu mwambie bidada kuwa unamuachia nyumba unaenda zako....
 
Mkubwa sheria inavigezo vyake mpaka umpe mtu talaka, na mahakama haipo kwa ajili ya kutenganisha ndoa, cha msingi tengeneza saikolojia yako kama kweli we n mkristo hlo swala mbna dogo sana lipeleke msalabani, au ukiona taabu sana kwa maana unataka msaada wa kisheria kwa wakili unalipiwa, so kwa kukusaidia kabla hjawaza kuachana hebu jarbu kumwona jamaa moja anatiwa Mr Mauki au aunt Sadaka atakusaidia kisaikolojia.
Nashukuru saana, naomba mawasiliano yake.
 
Back
Top Bottom