Msaada wa kisheria kwa huyu dada

Kwanza uchumba wa miaka mitano bila kuolewa ni dhambi isitoshe alikubalije kulala na huyo mwanaume kabla ndoa....anatakiwa akatubu kwanza kwa Mungu muumba mbingu na nchi, kisha atulie lakini pia akijiua ni dhambi nyigine ambayoitampeleka moja kwa moja kuzimu kuisubiri mauti ya Pili .
Mwambie anitafute mm nitamsaidia
 
Afanye mengine tu, hakuna kifungu cha sheria wala cha kidini kitakachomkatisha dr kufunga ndoa na amtakae
 
Mtoto abaki na mama. Baba atoe matumizi.

Aangalie haki ya mtoto pindi wazazi wanapotengana Sura ya 29

26.-(2) Kutakuwa na dhana isiyopingika kwamba itakuwa ni kwa maslahi ya mtoto aliye na umri wa chini ya miaka saba kuishi na mama yake isipokuwa katika kuamua kwamba dhana hiyo inafaa kutumika katika shauri husika, mahakama itazingatia kutosumbua maisha ya mtoto kutokana na kubadilisha makaazi yake.

Link hii hapa chini

http://masasitc.go.tz/uploads/files/SHERIA YA MTOTO YA KISWAHILI MWAKA 2014-1.pdf
 
Mpe pole sana..atakua anaumia sana...
Mimi namshauri atulize akili na wala asiumize kichwa kuzuia jamaa asioe coz hata akiweka pingamizi, haisaidii coz juyo jamaa hampendi tu na hata muoa...
Kwanza amshukuru Mungu kwakumpatia watoto wake wawili na amemuepushia mabaya ambazo zingemtokea badae...Siku zote Mungu ana sababu kwa tunayoyapitia..Sometimes Mungu akitaka kukuepusha na jambo baya mbele yako..atapitia njia yeyote even if it hurts bt that the only way you can be saved...
Amwombe Mungu ampe moyo wa uvumilivu na kusamehe..
Mwisho aende ustawi wa jamii na jamaa aitwe wapange namna ya kuwatunza watoto wake.
Wala asimtishe, mtoto mpaka afikishe miaka 7 ndo anaruhusiwa kumchukua lakini pia watapanga namna ya kumtembele mtoto.
Mungu amtie nguvu..
 
Mwambie aende ofisi za ustawi wa jamii zilizo karibu yake.

Watoto huyo jamaa hatoweza kuwachukua wala asiwe na wasi mpaka wafikishe miaka saba na watachagua pakwenda... Na ataendelea kutoa matunzo kama kawaida.
 
Kama ni Mkatoliki anaweza kuwela pingamizi cjui kwa madhehebu mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…