MSAADA WA KIAFYA.

Chimbekeha

JF-Expert Member
Dec 1, 2018
1,193
2,163
Habarini wapendwa wa JF,pole na majukumu ya kila siku,

Husika na kichwa cha habari hapo juu

Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka takribani 24,
nimekuja kwenu kwa kuamini nyie ni wajuzi wa mambo yahusuyo afya,
Tatizo langu ni kwamba Tangia mwaka 2016 ninasumbuliwa na tatizo la fangasi sugu katika sehemu ya siri, fangasi hiyo hujenga tabaka la MAGAMBA sehemu ya juu ya korodani zote mbili, hali ambayo mda mwingine hupelekea michubuko midogomidogo inayoweza hata kubadilisha mwendo wangu ninapotembea, hadi kufikia leo nimetumia sabuni na dawa tofauti za kuzuia au kutibu hali hii ila badala yake inapungua tu na sio kupona kabisa, dawa za kuna kupaka zote zimetumika ila husaidia pale unapopaka tu na hatimaye ukakasi hurudi katika hali ya mwanzo.
Ni matumaini yangu kuwa nimejieleza kiasi cha mtu kupata taswira ya hali halisi.

KUMBUKA; sijawahi ugua ugonjwa huu kabla na chanzo chake ni maji ya chemchem ilio kubwa ambayo tulikuwa tunaitumia kupikia na kuoga kutokana na uhaba wa maji chuoni wakati nachukua fani fulani..

Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo matibabu ya fungus yanachukua muda si chini ya wiki sita na kuendelea, wakati mwingine unaweza kulazimika kutumia dawa kwa miezi kadhaa! Wengi hili linawashinda akimaliza tube moja hajaona nafuu either anaacha dawa au kubadili hospital, nakushauri ufanye yafuatayo:

1. Tafuta daktari bingwa wa ngozi ( dermatologist) atakusaidia, kama hilo haliwezekani

2. Nunua CLOTRIMAZOLE POWDER ( sio cream) utumie kutwa mara mbili asubuhi na jioni kila unapooga kwa miezi 2 hadi mitatu Pamoja na vidonge vya FLUCONAZOLE 150 mg utumie kimoja kwa siku kwa wiki 4

3. Zingatia sana usafi wa mwili, oga asubuhi na jioni na ubadili nguo za ndani ( boxer) kila siku, na hizo boxer ikiwezekana ziwe 100% cotton na ukizifua zianike kwenye jua kali zikauke vizuri kabla ya kuvaliwa

Cha kuzingatia usitegemee matokeo ya haraka , itachukua wiki kadhaa kabla hujaanza kuona mabadiliko

Asante mkuu kwa ushauri wako nitaufanyia kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wadudu ni sugu kweli, ila nashukuru sasa tofauti na mwanzo michubuko na magamba yote yamepotea mkuu
 
Back
Top Bottom