Msaada wa haraka unahitajika kuhusu kilimo cha mtama

mwasita

JF-Expert Member
Aug 5, 2016
371
376
Kwa wataamu wa kilimo naombeni msaada wenu niweze kusaidia jamii ya wakulima wa kijijini kwetu na maeneo jirani kwa watakaokubali ushauri ntakaowapa kutokana na majibu yenu!

Kutokana na hali ya ukame ulioyakumba maeneo makubwa ya nchi yetu ni dhahiri kuna kila dalili ya kuwepo kwa upungufu mkubwa wa chakula ambao kwa umri wa watu wa rika langu hatujawahi kuushuhudia! Mpaka sasa debe la mahindi kijijini kwetu linanunuliwa Tsh 20000 kitu ambacho sijawahi kushuhudia maishani mwangu!

Mazao waliyokuwa wamelima wakulima hawa nayo yameshaanza kunyauka hasa yaliyo maeneo yasiyotunza unyevu kwa mda mrefu. Lakini pamoja na hayo kwa sasa kuna dalili za mvua kurudi kwani zimeshaanza japo kunyesha kidogo kidogo!

Nawaonea huruma wakulima hawa hasa wanaotegemea kilimo pekee bila kuwa na nyenzo zingine za kupata japo pesa ya kununulia chakula hata kama kitatoka maeneo mengine! Kutokana na mvua kuanza kunyesha nataka niwashauri wakulima hawa wasikate tamaa badala yake walime mtama pengine mvua itanyesha kwa mda mrefu hivyo utawasaidia!

Swali langu kwenu;
Ni mbegu ipi ya mtama ambayo unaweza kuipanda ikakomaa kwa mda mfupi? Naomba kujua ili ninapowapa ushauri niwatajie na aina ya mbegu moja kwa moja!
Ahsanteni!
 
Huu Uzi Wa maana sana, nami nipo kusubiri wataalamu hapa. Ngoja niweke kigoda changu vizuri....
 
Back
Top Bottom