Msaada wa haraka: Je, ujauzito huu umeharibika?

the muter

JF-Expert Member
Oct 31, 2012
1,330
1,799
Mke wangu alipata mimba mwezi wa 11. Mwanzoni mwa mwezi wa 12 aliumwa sana tumbo na damu zilimtoka karibu wiki nzima.

Binafsi nilidhani ni miscarriage (mimba kuharibika), ila toka juzi kajisikia maumivu ya kiuno na leo kaenda Hospitali kaandikiwa dawa kama 4 tofauti.

Nimesoma mojawapo ina tahadhari kwa wajawazito. Nikamwambia wife akanunue kipimo cha mkojo apime kwanza kwani mwanzo tuliamini ni miscarriage. Baada ya kupima mimba inaonekana ipo.

Je, inawezekana miscarriage itokee December 6 mpaka leo kipimo bado kioneshe mimba? Dalili nazo za mimba zimeisha pia.

Mawazo yenu wadau kabla sijamwanzisha dozi..
 
Alivopata bleed mlienda hospitali? Mliambiwa kapata miscarriage? Inatokeaga kubleed wakati wa ujauzito japo sio dalili nzuri.....vitu sensitive kama hivi ni vema mkawahi hospitali
 
Alivopata bleed mlienda hospitali? Mliambiwa kapata miscarriage? Inatokeaga kubleed wakati wa ujauzito japo sio dalili nzuri.....vitu sensitive kama hivi ni vema mkawahi hospitali

Tulikwenda ila daktari alisema mtu wa vipimo hayupo ila alimwandikia doz ya cipro nadhan
 
vipi kuhusu lishe yake?

Anakula vizuri, Mara nyingi asubuhi huwa tunatumia uji wa lishe, Milo 3 , matunda pia. Ananizidi hata mm kula.labda miaka 3 nyuma akiwa Chuo lishe ilikuwa mgogoro hata mwili ulikuwa tofauti
 
Mara ya kwanza hamkufanya kipimo cha mimba akapigwa cipro bila kuambiwa tatizo na mkarudi bila kujua mimba ipo au imetoka, kwa nini hamkwenda hosp nyingine ili muwe na uhakika??
Mmerudi mara ya pili mmepewa dawa aina 4 ina maana hamjaambiwa ni za nini?? Kapewa izo dawa bila vipimo hasa cha mimba??? Samahani kwa maswali mengi ila mnatakiwa kuwa makini na ishu sensitive kama hizo, rudini hosp kama hamuelewi mnatibu nini na izo dawa.
 
ni vizuri ukamtafuta Dr.wa wanawake na watoto angekusaidia lasivyo itazidi kuwa mbaya hadi kupelekea mimba kuharibika kwasababu ya upungufu wa damu utakao endelea,na tulio wengi hatuna elimu ya uzazi.
 
Back
Top Bottom