Msaada wa file loading

Papaa Kinyani

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2013
Posts
1,457
Reaction score
699
Wandugu naombeni msaada ya ku-load files kubwa kubwa mpaka 1GB kwenye net na kuweza kumtumia mtu mfano nje ya nchi na yeye aweze ku-download kirahisi. Je kuna software maalum au nifanyeje? Maana hivi vi-modem vyetu mwisho ni 25MB, sasa kama una zaidi ya hapo je? Msaada wandugu!!! Keep waiting for help!!!


Sharing is Caring
 
yakuspaa kuwa na elimu kidogo juu ya file format na unatumia njia gani kutuma hilo file,kama unatumia e-mail kunakuwepo limitation kati ya aina moja ya account mfano yahoo,gmail,hotmail n.k.hivyo sio laisi kutuma kiwango kikubwa cha data bila idhini yao.lakini kuna jia nyingine ya kawaida unaweza kutumia nayo ni kucopress hilo file kwa kutumia software maalum hivyo kukuwezesha kulipunguza ukubwa wake na likishakutumwa mpokeaji atatumia software pia kulipata kwa kiwango ulichodhamilia.
 
Njia pekee ni ile ya kuweka makabrasha(files) yako "online" na wao kukupa link ambayo ukiwa mahali popote palipo na huduma ya mtandao, unaweza kupakua(download) makabrasha yako uliyoyapakia(upload) hapo awali.
Njia nzuri ya kutumia huduma hii ambayo huwa ni ya bure, unahitaji kuvunjavunja hilo kabrasha lako lenye "size" kubwa na kulifanya vipande vidogo vidogo ili iwe uweze kupakia na kupakua kwa urahisi.
Software nzuri ya kuvunjavunja kabrasha kubwa na kuwa vipande vidogo vidogo ni 7-Zip na unaweza kudownload HAPA

Kwa maelezo zaidi ya namna ya kufungua Account ya SkyDrive fuatilia hapa:
Microsoft SkyDrive - Microsoft Windows

Pia jaribu kufuatilia kwenye mitandao mingine ifuatayo ambayo pia hutoa huduma kama hii.

www.dropbox.com - inatoa 2GB na kujiunga ni bure.
www.sugarsync.com - inatoa 5 GB kujiunga ni bure.
www.zumodrive.com - inatoa 1 GB kujiunga ni bure.
www.spideroak.com - inatoa 2GB kujiunga ni bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…