Zimpombe
Member
- Aug 9, 2016
- 28
- 24
Habari wanaJF
Nimesumbuliwa sana na minyoo mwaka jana. Hadi kuja kugundua kuwa ni minyoo, ni baada ya kuwa napata kichefuchefu mara kwa mara baada ya kula au kabla ya kula, najikuna sana sehemu za ugoko za miguu yangu yote miwili, tumbo kunisumbua mara kwa mara samba na miungurumo ya sauti nyembamba ikiwemo na, na kiasi fulani kupungua mwili.
Kabla yakwenda kupima, nilikwenda Pharmacy moja kununua albendazole(kama nimekosea jina naomba kusahihishwa) za kampuni ya Zentel ambayo niliambiwa ni ya Suoth Afrika, vidonge vitatu kwa na meza kwa siku 3 Sh 15,000/= , kwamba vina nguvu sana ndio maana bei ghali. Nilitumia, sikuona mafanikio, ni kama nilitibua hali.
Nilichukua uamuzi wa kwenda kupima Dispensary moja kubwa, nikaambiwa nina minyoo mingi. Hivyo nikamwambia Doctor dawa nilizokuwa nimetumia hapo kwanza. Hivyo akanipa albendazole vidonge vitano vya kumeza siku tano kila asubuhi, sambamba na vidonge vingine(antibiotics) vya kumeza siku 10(sivikumbuki jina) na akanipa masharti kuwa nisitumie vyakula vichachu, vya protini, na vya mafuta kwa hizo siku. Badaa ya hapo, huo mwezi wa kumi hali ikawa shwari.
Jambo lililonifanya kuomba msaada, ni hali ile imejirudia tena. Je, ni dawa gani nitaweza kuikomesha minyoo hii? Naamini msaada wenu, utakuwa msaada kwa wengine pia.
Asante.
Sent using Jamii Forums mobile app